July 14, 2020

JOYCE KIRIA "ALIA" NA MFUMO DUME MIKOA YA KASKAZINI


Mwanaharakati wa Haki za Wanawake nchini, Joyce Kiria.



Na Mwandishi, Wetu -Kilimanjaro


MWANAHARAKATI wa Haki za Wanawake nchini Joyce Kiria amitaka jamii ya Kanda ya Kaskazini kuacha tabia ya kuendekeza mfumo Dume katika kipindi hiki tunapoelekea Uchaguzi Mkuu huku akiwataka wanawake kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi 

Kiria alitoa kauli hiyo jana mkoani Kilimanjaro wakati akitoa pongezi kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kumpitisha Dkt John Pombe Magufuli kwa asilimia 100 kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

mbali na pongezi hizo kwa wajumbe Kiria pia amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kukiwakilisha chama cha Mapinduzi katika nafasi ya Urais na namna ambavyo ametoa nafasi kwa Wanawake kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

,Kiria alisema mafaniko na kazi kubwa alizofanya Rais Dkt Magufuli kwa kasi kikubwa zimechangiwa na imani aliyoionesha kwa kundi la Wanawake katika kumsaidia kutekeleza majukumu yake.

“Wanawake tumeonyesha mchango mkubwa sana ,hata katika utumbuaji tumeona wanaume ni wengi ,wanawake tumesimama japo kwa uchache wetu lakini tumeweza kumsaidia Rais ,hivyo nawahamasisha wanawake hasa wa kanda hii ya kaskazini tujitokeze kwa wingi kwani uwezo tunao wa kuchapa kazi na kuijenga Tanzania,”alisema Kiria

Aliwataka Wanawake wa kanda ya kaskazini kutomuangusha Rais Magufuli katika harakati za uchaguzi huku akitoa wito kwa wananwake wengi zaidi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali kwani ni rahisi kwao kupata ushindi ukilinaganisha na wanaume.

“Niwaombe wanawake wa kanda ya kaskazini tusimwangushe Rais wetu tujitokeze kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali,na tunaamini wanawake wakigombea ni rahisi kushinda, tunajua ukanda  huu wa kaskazini kuna mfumo dume lakini kina baba  jitahidini kuonyesha imani yenu kwa akina mama kama ambavyo Rais alivyotuamini na kupongeza kazi kubwa zilizofanywa na wanawake,” alisema Kiria.

Kiria ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki kwa Wanawake (HAWA) alisema ni wakati  wa hamasa kwa wanawake  kwenda kumsaidia Rais Magufuli kuijenga nchi  ili kumpunguzia kazi aliyoifanya mara kwa mara ya kutengua na kuteuabadala kushughulikia mambo mengine makubwa zaidi ya nchi.

“Sasahivi tunaona nchi yetu imeingia kwenye uchumi wa kati na hivyo utaenda kwenye uchumi wa juu zaidi,…ataka niwambie wanawake Rais wetu anatuamini sana hata tukiona watendaji wake ambao wengi ni wanawake wamekuwa wakifanya kazi kwa weledi bila kumuangusha Rais wetu mpendwa,ni dhahiri kwamba wanawake
tunaweza” alisema Kiria.

No comments:

Post a Comment

Pages