Eng.Ezra Chiwelesa Kushoto mgombea ubunge jimbo la
Biharamuro CCM akimkabidhi Fomu Katibu wa CCM Wilaya ya Biharamulo Bi Adia
Rashid Mamu Kulia baada ya kuichukua fomu hiyo julai 14 mwaka huu dirisha la
uchukuaji fomu lilipofunguliwa rasmi na kuirejesha leo julai 15,mwaka huu akiwa
ameijaza.
Na Allawi Kaboyo, Biharamulo
Ikiwa ni siku ya pili ya kuchukua na kurejesha fomu
za kugombea ubunge na udiwani kwa wanachama wa chama cha mapinduzi kote nchini,
waliochukua fomu za kugombea ubunge wa jimbo la Biharamulo sasa wafikia 40 ambapo
7 kati ya hao ni wanawake.
Hayo yamebainisha leo na Bi Adia Rashid Mamu katibu
wa ccm wilaya ya Biharamulo alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ofisini
kwake kwa lengo la kueleza mwenendo mzima wa uchuaji fomu unavyoenedelea
wilayani humo.
Bi Adia ameeleza kuwa wananchama katika wilaya hiyo
wamehamasika na kujitokeza kutekeleza haki yao ya kikatiba kama wananchama na
kuongeza kuwa hamasa hiyo inatokana na mambo makubwa yaliyofanywa na serikali
ambayo ipo chini ya chama chao ikiongozwa na Rais Magufuli.
Amesema kuwa uchukuaji wa fomu za ubunge umegusa
rika zote huku akionyesha kufurahishwa na wingi wa wananwake waliojitokeza
kugombea jimbo hilo pamoja na vijana na kuwataka watia nia hao kufuata kanuni
na taratibu za chama na kuongeza kuwa licha ya idadi hiyo kuwa kubwa mbunge
aliyemaliza muda wake bado hajajitokeza kuchukua fomu.
“Mwenendo
wa uchukuaji fomu za ugombea hapa kwetu unakwenda vizuri na wanachama
wamehamasika kwa wingi kuchukua fomu, kinachonifurahisha Zaidi ni kuona
wanawake na vijana wamejitokeza hili linaashiria kuwa ndani ya chama chetu
demokrasia imetawala na kuonyesha uongozi sio wa watu Fulani. Niwaombe
wananchama waendelee kujitokeza kuja kuchukua fomu maana fomu zipo na gharama
yake ni shilingi laki moja ambapo mgombea anaweza pia kutoa mchango wa hiari
kwaajili ya kuchangia chama katika mchakato mzima wa kampeni.”
Amesema Bi Adia
Aidha katibu huyo amesema kuwa maandalizi kuelekea
kwenye kura za maoni yapo vizuri ambapo amebainisha kuwa katika wilaya hiyo
wapo Zaidi ya wajumbe 600 ambao wote wanatarajia kushiriki kikamilifu uchaguzi
huo ndani ya Chama na hatimaye wakampata mgombea atakayepeperusha bendera ya
CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba mwaka huu.
Nje ya ofisi hiyo walikuwepo baadhi ya watia nia
ambao walikuwa wananendelea kuchukua fomu na wengine wakirudisha fomu ambao
miongoni mwa wagombea hao ni Mhandisi Ezra Chiwelesa ambaye amefika ofisini
hapo kurejesha fomu na kuwaeleza waandishi wa habari kuwa yeye kama kijana
ameamua kugombea ubunge ili kuwatumikia wanabiharamulo.
Ezra ameongeza kuwa mfumo uliopo ndani ya chama chao
unaweka uhuru wa kila mwananchama kugombea hivyo ameamua kuja Biharamulo kuweza
kukabiri baadhi ya changamoto ambazo kwazo zimekuwa kero ya muda murefu kwa
wananchi wa wilayao hiyo.
“Nimeamua
kuchukua fomu ya kuomba kugombea nafasi ya ubunge kupitia chama change nikiamini
mimi na weza kuwatumikia wananbiharamulo, chama chetu sasa ni kipya na mimi
nataka Biharamulo yetu iwe mpya na iwe sehemu ya kuwavutia wawekezaji maana
tayari tunayo mbuga inayopita kwenye wilaya yetu ya BURIGI CHATO hii ni fursa
kwa wananchi wa Biharamulo.” Amesema Mhandisi Ezra.
Ameeleza kuwa katika mchakato wote anawasihi watia
nia wenzake kutotumia Lugha chafu kwa wagombea wenza na kuwataka wajumbe
kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwa kushawishiwa na baadhi ya wagombea na
kuwapa vijisenti ili wawachague huku wakijua wanatangeneza mstakabali wa maisha
yao ya miaka mitano ijayo.
Mwingine aliyekuwepo ni Bw. Idrissa Songoro ambaye
naye amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea ubunge wa jimbo
hilo ambapo ameeleza kuwa kutokana na demoklasia iliyopo ndani ya chama
anajiona anatosha kuwatumikia wananbiharamulo.
Katika wilaya ya Missenyi waliojitokeza kuchukua
fomu za kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Nkenge wafikia 46 hadi julai 15
mwaka huu ambapo miongoni mwa watia nia hao wamo waliowahi kuwa wabunge wa
jimbo hilo ambao ni Balozi Dkt. Deodorus Kmara mbunge aliyemaliza Muda wake,
Mhe.Asumputa Mshama aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa Katibu wa chama hicho wa wilaya
Missenyi Emanuel Alex ameeleza kuwa miongoni mwa watia nia hao wane kati ya hao
ni wananwake huku akizidi kuhamasish wananchama kwenda kuchukua fomu ili waweze
kukipigania chama chao.
Aidha kwa upande wa Jimbo la Ngara watia nia
waliochukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM
wafikia 39 hadi julai 15 mwaka huu huku mmoja kati ya hao ni mwanamke.
Kwamujibu wa katibu wa ccm wilaya ya Ngara Mapanga
Nelele amesema kuwa mwenendo wa uchukuaji fomu unakwenda vizuri ambapo ameeleza
kuwa miongoni mwa watia nia hao yumo mbunge aliye maliza muda wake Mhe. Alex
Gashaza ambaye nay eye amechukua fomu kwaajili ya kuitetea nafasi yake ambapo
ameongeza kuwa waliochukua fomu kuwania udiwani viti maalumu wamefikia 16.
Nelele amewasihi wagombea kuendelea kufata kanuni na
taratibu za chama katika mchakato mzima ili waweze kuenzi katiba ya chama chao
na kuwasihi wanachama kuendelea kuzitumia siku zilizobakia kujitokeza kuchukua
fomu.
No comments:
Post a Comment