Injinia Athuman Mfutakamba (kulia), akipokea
fomu jana ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge wa Jimbo la Igalula kutoka kwa
Katibu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Uyui Neema Lunga (kushoto).
Mtaalamu wa Maabara kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(uyui) Joseph Gibuya akimkabidhi Kaimu Katibu wa Wilaya ya Tabora Violet Kassanga fomu kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge wa Jimbo la Tabora Mjini mara baada ya kukamilisha kuijaza.
Shaffir Sumar (kshoto) akipokea fomu jana ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini kutoka kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Uyui Neema Lunga(kulia).
Mussa Ntimizi (kushoto) akipokea fomu jana ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge wa Jimbo la Igalula kutoka kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Uyui Neema Lunga(kulia). (Picha na Tiganya Vincent).
NA TIGANYA VINCENT
MAKADA mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi katika majimbo ya Wilaya ya Tabora na Uyui wazidi kuchukua na kurudisha fomu za kuomba kuteuliwa kugombea ubunge kwa tiketi chama hicho.
Kaimu Katibu wa Wilaya ya Tabora Violet Kassanga alisema katika jimbo la Tabora Mjini , jumla ya wagombea 32 walikuwa wamechukua fomu ikiwa wanawake 3 na wanaume 29.
Alisema kuwa hadi mchana Makada 10 akiwemo Mtaalamu wa Maabara kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(uyui) Joseph Gibuya walikuwa wamerejesha fomu za kuomba kuteuliwa.
Kwa upande wa Katibu wa Wilaya ya Uyui Neema Lunga alisema hadi kufikia leo jumla ya wanachama 25 wa Majimbo ya Tabora Kaskazini na Igalula walikuwa wamechukua fomu.
Alisema katika jimbo la Igalula wanachama 6 wamejitokeza kuomba kuteuliwa na Tabora Kaskazini walikuwa wamejitokeza wanachama 19.
Miongoni mwa waliojitokeza kuomba kuteuliwa katika Jimbo la Tabora Kaskazini ni aliyekuwa Mbunge mwaka 2010 hadi 2015 Shaffir Sumar na Mbunge aliyemaliza muda wake Almas Maige.
Kwa upande wa Jimbo la Igalalu wanaomba ni pamoja na aliyewahi kuwa Mbunge wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne Injinia Athuman Mfutakamba na Mbunge anayemaliza muda wake Mussa Ntimizi.

No comments:
Post a Comment