Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Charles Kichere, akioneshwa kitabu cha
bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 toleo la wananchi, na Afisa wa
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Juma Mfaume wakati alipotembelea banda la Wizara
hiyo katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es
Salaam ambapo Wizara ya Fedha na Mipango na Taasisi zake inashiriki katika maonesho
hayo kwa lengo la kuwafikia wananchi na kutoa elimu na huduma mbalimbali.
.Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), Bw. Msafiri Mbibo akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa
wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Juma Mfaume, alipokuwa akitoa elimu
kuhusu bajeti ya Serikali na namna Serikali inavyosimamia mchakato wa uandaaji
na utekelezaji wa bajeti. Katikati ni Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa
Mamlaka hiyo Bw. Richard Kayombo.
Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw.
Msafiri Mbibo akimsikiliza Bw. Hassan Mwakioja, alipokuwa akitoa elimu kuhusu
sera za uchumi jumla na sera za kibajeti na namna Serikali kupitia Wizara ya
Fedha na Mipango inaziwezesha Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali
na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuendesha shughuli zake na kukusanya maduhuli
ya Serikali, wakati wa Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea
katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge Bw. Stephen Kagaigai, akisikiliza
maelezo kutoka kwa Afisa wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Joseph Msumule
alipokuwa akieleza Sera, Sheria na kanuni za huduma ndogo za fedha zenye lengo
la kuweka mazingira wezeshi ili kurahisisha usimamizi wa huduma ndogo za fedha
katika sekta ya fedha, kutoa elimu kuhimiza watoa huduma ndogo za fedha waweze
kujisajili na kupata leseni, katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea
katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge Bw. Stephen Kagaigai, akisikiliza
maelezo kutoka kwa Afisa wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Maendaenda,
alipokuwa akitoa maelezo kuhusu Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki
(GePG) wenye lengo la kuongeza uwazi na udhibiti wa fedha za umma, kuboresha na
kurahisisha namna ya kulipia huduma za umma, katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa
ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere jijini
Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge Bw. Stephen Kagaigai, akisaini daftari
la wageni alipotembelea banda la
maonesho la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya
Biashara yanayoendelea katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Afisa wa Wizara hiyo Bi. Josephine Majura.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), Bw. Msafiri Mbibo akimsikiliza Afisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano kwa
Umma wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Bi. Shamim Mdee,
alipokuwa akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa na Bodi hiyo, wakati
alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara
yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Charles Kichere, akimsikiliza Mchambuzi wa Mifumo
wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bi Siganike Baruti, alipokuwa
akitoa elimu kwa umma wakati wa Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara
yanayoendelea jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara
ya Fedha na Mipango).
No comments:
Post a Comment