HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 07, 2020

VETA DODOMA YAWATAKA VIJANA KUJIKITA KATIKA MAFUNZO YA UFUNDI


Na Tatu Mohamed

CHUO cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dodoma, kimetoa wito kwa vijana nchini kuacha kukaa mtaani badala yake kujikita na mafunzo ya ufundi ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza katika maonesho ya 44 ya Biashara ya kimataifa ya Sabasaba, Mwalimu wa Chuo hicho Dodoma, Dayosta Mshori amesema  vijana wanapaswa kujitoa na kujituma ili kuweza kufanikiwa katika maisha yao.

Mshori amesema Chuo cha Veta kimekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana katika kuwainua kifani na kuwafikisha sehemu ambayo wanaweza kujisimamia.

Amesema wamekuwa wakiwapokea vijana wakiwa ngazi ya chini na kuwaelekeza fani mbali mbali ambazo baadae wanakuja kuchagua zile zinazowafaha katika kujifunza zaidi.

"Tunawajengea uwezo vijana kujifunza katika mafunzo mbalimbali na tukigundua kama wanakipaji cha ubunifu tunawasaidia kuwaendelezea  kutimiza ndoto yao," amesema na kuongeza

"Kuna baadhi ya vijana ambao tumewasapoti akiwemo Mbunifu wa Pikipiki iliyotumia mashine ya kumwangilia na baadhi ya vifaa vya baskeli ambayo veta imemsaidia hadi kuikamilupisha," amesema

Kwa Upande wake Mbunifu wa Pikipiki, Simon Njovu amesema mwanzo alipokuwa anaingia veta kupata mafunzo aliona fursa ya kutumia ubunifu wa kutengeneza kifaa cha usafiri Pikipiki.

Amesema Pikipiki hiyo ametengeneza kwa kutumia vifaa vya hapa hapa nchini na zinauwezo wa kumsaidia mtu katika safari zake.

No comments:

Post a Comment

Pages