July 21, 2020

VIJANA WANAOINGIA KATIKA SIASA WAASWA KUWA WAVUMILIVU NA WENYE NIDHAMU

Wakazi wa Wilaya ya Kilosa,mkoani Morogoro wameatakiwa kuanza kufikiria namna bora ya kuleta maendeleo katika jimbo hilo badala ya kutumia muda mwingi katika migogoro na kuridhika na vitu vidogo wanavyopewa na wanasiasa baada ya kuwachagua.

Hayo yamesemwa na mtia nia wa ubunge katika jimbo la Kilosa aliyeibuka kidedea katika kura za maoni Prof. Palamagamba John Kabudi alipokuwa akitoa shukrani zake mara baada ya kuchaguliwa na wana ccm wenzake katika kinyang’anyiro cha kura za maoni kupitia chama cha mapinduzi jimbo la Kilosa.

Kabla ya kutangaza matokeo hayo yaliyoendeshwa kwa njia ya uwazi msimamizi wa uchaguzi huo Bw Mohamed Mzee amesema yeye hana mamlaka ya kumtangaza mshindi bali anamtangaza aliyeongoza kwa kupata kura nyingi huku akiwaasa vijana kuwa wavumilivu na wenye nidhamu wanapoamua kuingia katika siasa.

Uchaguzi wa kura za maoni kupitia Chama cha Mapinduzi katika jimbo la Kilosa ulikuwa na watia nia 29,ambapo kura 1013 zilipigwa na wajumbe waliohudhuria ambapo kura tano ziliharibika ambapo katika kura hizo aliyeongoza ni Prof. Palamagamba John Kabudi aliyejizolea kura 714,Mshindi wa pili Bw. Kaunda Alfat Saidi amepata kura 101 na mshindi wa tatu amepata kura 51.

No comments:

Post a Comment

Pages