KUTOKANA na ongezeko la watu na maendeleo ya viwanda jiji la Dar es Salaam linakadiriwa kuzalisha taka tani 12,000 kwa siku ifikapo 2025.
Pia taka ni fursa wananchi wanapaswa kuzitenganisha ili iwe rahisi kurejelezwa kwa matumizi mengine.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa mazingira uliowakutanisha wadau na serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazohusiana na udhibiti wa taka za majumbani, taasisi na hospitali.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dk. Samuel Gwamaka, alisema sasa inakisiwa kuwa hadi kufikia mwaka 2025 Dar es Salaam pekee inaweza ikakusanya taka hatarishi na zingine tani 12,000.
Alisema ni changamoto ambayo imekuwa ikikua kutokana na ongezeko la watu na maendeleo ya viwanda.
Alisema mpango huo wa utenganishaji taka na kuzirejeleza utakuwa endelevu utakaohakikisha mazingira yanaboreshwa na kuondoa changamoto hizo.
Alisema hadi sasa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 inazitaka kila Halmashauri, Jiji na Manispaa kuweka mfumo wa kutenga taka kuanzia zinapozalishwa.
Sheria hiyo inampa mamlaka Waziri wa Mazingira kuweka muongozo wa namna ya kutenga taka hizo kwani taka hizo ni fursa endapo zitarejelezwa kwa kuleta ajira, kupunguza uletaji wa malighafi kutoka nje.
“Unakuta zile taka unazozalisha kuwa fursa ya kuweza kuendeleza hata kwenye uchumi wa viwanda na kupunguza uletaji wa malighafi nyingi kutoka nje,”alisema.
Aliongeza kuwa kunahitajika kuwa na mfumo ambao utahakikisha mazingira yanatunzwa na wadau wanashirikiana kuhakikisha mazingira yanaboreka na kushusha gharama za ukusanyaji taka.
Aliongeza kuwa maendeleo yanavyozidi kupatikana ndivyo changamoto zinaongezeka na kuwaasa wananchi kutenganisha taka za vyakula, chuma na plastic na kuuza.
“Kutenganisha taka zinapozalishwa isichukuliwe mzigo inaweza kwa wenye taka ili wajipatie kipato na wanaokusanya kutoa unafuu kwa kujipa ajira,”alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Tindwa Medical & Health Services (TMHS),Dk. Chakou Halfan alisema kuna tatizo la taka nchini linalohitaji kutatuliwa.
“Tumechelewa sana kwani kwa sasa Dar es Salaam inazalisha taka tani 10,000 kwa siku miaka mitano ijayo itakuwa tani 12,000 kwa siku, tungeanza hili zamani sana lakini tumona tupate ruhusa wa wadau wa mazingira kuhakikisha changamoto hizi tunazikabili,”alisema.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Jielimishe kwanza, Henry Kazula alisema alisema wamekuwa wakifanya mafunzo ya uhifadhi wa taka kwa jamii kuwa ni jukumu la kila mmoja.
“ Jamii inatakiwa kuzichukulia taka kama fursa , kuzitenganisha taka katika eneo wanazozalisha ili kupunguza uzalishaji wa taka nyingi maeneo ya dampo,”alisema.
No comments:
Post a Comment