Na Asha Mwakyonde
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imefungua dirisha la udahili wa Shahada ya kwanza kwa awamu ya kwanza kwa mwaka 2020 badala ya Agosti 31, mwaka huu.
Pia imewataka wawaombaji wa udahili kuhudhuria maonesho ya 15 ya Elimu ya juu, Sayansi na Teknolojia yatakayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja kuanzia Agost 31 hadi Novemba 5 mwaka huu.
Hayo yalibainisha jana jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji, Dk.
Charlse Kihampa baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha sita hivi karibuni.
“Tume inaendelea kuwahimiza waombaji wote wa udahili kuendelea kupata taarifa rasmi kupitia tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz), tovuti za vyuo vilivyoruhusiwa kudahili wanafunzi wa Shahada za kwanza,”alisema.
Alisema pia kufuatilia taarifa mbalimbali zinazotolewa na tume hiyo kupitia vyombo vya habari.
Alisema udahili wa kujiunga na Shahada ya kwanza utahusisha makundi matatu ambayo ni wenye sifa stahiki za kidato cha sita, wenye sifa stahiki za Stashahada au sifa linganifu pamoja na wenye sifa stahiki za foundation program ya Chuo Kikuu huria cha hapa nchini.
Dk.Kihampa alisema maombi yatumwe moja kwa moja kwenye vyuo ambavyo muombaji amechagua na kuchagua program za masomo anazozipenda.
Alitoa wito kwa waombaji wa Shahada ya kwanza endapo wanahitaji kupata ufafanuzi wa suala linalohusu udahili wawasiliane na vyuo husika moja kwa moja.
“TCU inawaasa wananchi kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala na washauri wanaodai wanatoa huduma ya namna ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu hapana nchini,”alisema.
No comments:
Post a Comment