HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 02, 2020

WAZEE WANATAKIWA KUTAZAMWA KWA JICHO LA KIPEKEE

 

Na Lydia  Lugakila Muleba

Wazee wilayani Muleba Mkoani Kagera wameiomba halmashauri mkoani humo kuagiziwa dawa za kutosha kulingana na magonjwa yanayowasumbua.

Kauli hiyo imetolewa na na mmoja wa wazee hao Perpetua Nsabi, katika maadhimisho ya siku ya wazee yaliyofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Ndalichako  kata ya Rulanda wilayani humo.
 

Nsabi amesema kuwa licha ya Serikali kutoa msamaha wa matibabu bure kwa wazee hao,  bado sauti zao hazisikilizwi mara kwa mara hivyo wanahitaji kutazamwa kwa jicho la kipekee na kwa vitendo ili   kuondokana na kupata matibabu kwa shida.

Amesema kuwa wazee wengi wanapokwenda kutibiwa katika taasisi za afya serikali na za umma Mara nyingi madawa ya magonjwa yanayowasumbua yamekuwa  hayapatikani kwa hivyo uambulia neno NENDA KAJINUNULIE Jambo ambalo amesema linakinzana na mpango na maelekezo ya serikali juu ya wazee wote kupatiwa matibabu bure, hivyo kuomba kuagiziwa dawa za kutosha ikiwa ni pamoja na kuanzisha utaratibu wa klinik kwa kata zote  zisizo na zahanati wala vituo vya afya ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya afya angalau Mara moja kwa Kila mwezi.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Faustin Kamuzora ambaye ni katibu tawala Mkoa wa Kagera amesema kuwa serikali Mkoani humo inatambua  haki za wazee na kuwa hatokubali  wazidi kunyanyaswa huku akiahidi kushughulikia changamoto zonazowakabili.

Katika sherehe hizo limezinduliwa Baraza huru la wazee ambapo Mwenyekiti wa mabaraza  huru ya wazee Mkoa wa Kagera Mzee Clement Kwezi Nsherenguzi amesema kuwa sera ya wazee ya mwaka 2003 ya taifa ni nzuri ukiisoma Ila utelekezaji wake wa kutungiwa Sheria umekuwa mgumu sana na kusababisha wazee kuendelea kunyanyaswa katika vituo vya vituo vya afya kukosa haki zao za msingi Kama matibabu na mafao yao.

Mzee Nsherenguzi ameongeza kuwa wazee hao wanapata matibabu kwa shida kutokana na kutokuwepo na Sheria ya kumlazimu Daktari kuhudumia wazee, huku akiiomba idara ya afya kufikilia namna ya kuweka wataalam wa afya ambao wamebobea katika magonjwa ya wazee ili watibiwe.

Hata hivyo bado jamii pia inahitaji kuwapa wazee huduma, ulinzi na utetezi ili wasijisikie wanyonge kutokana na matatizo ya kiafya kiuchumi, au msongo wa mawazo.

No comments:

Post a Comment

Pages