Mratibu wa Program ya Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya
Misitu (FORVAC), Emmanuel Msoffe akizungumza na waandishi wa habari
wanaoshiriki mafunzo kuhusu misitu, mazingira na uhifadhi wilayani
Ruangwa mkoani Lindi.
Waandishi
wa habari wakiwa kwenye mafunzo kuhusu misitu, mazingira na uhifadhi
yaliyoandaliwa na Program ya Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu
(FORVAC) yanayofanyika wilayani Ruangwa mkoani Lindi na Mkoani Ruvuma
kuanzia tarehe 27- Novemba hadi 2 Desemba, 2020.
PROGRAM
ya Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu (FORVAC) imetoa mafunzo kwa
waandishi wa habari zaidi ya 20 kutoka vyombo na mikoa mbalimbali
kuhusu uandishi wa Habari za Kiuchunguzi za Kimisitu (IJF) kwenye sekta
ya misitu ili kuchochea uhifadhi na maendeleo.
Mafunzo
hayo yametolewa na wakufunzi Cassin Sianga na Deo Mfugale kupitia
Programu ya FORVAC ambayo inatekelezwa na Idara ya Misitu na Nyuki
chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii .
Akizungumza
baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo Mratibu wa Kitaifa wa FORVAC,
Emmanuel Msoffe amesema wamekuwa wakitoa mafunzo kwa waandishi wa habari
ili kuwajengea uelewa kuhusu programu hiyo na misitu kwa ujumla kwa
ajili ya kuelimisha umma juu ya manufaa ya uhifadhi endelevu wa misitu.
Msoffe
amesema wanaamini kuwa waandishi wakiwa na uelewa wa faida na thamani
iliyopo kwenye misitu na mazao yake misitu kiuchumi, kijamii,
kimazingira na maendeleo endelevu wataweza kuandika habari nzuri za
kiuchunguzi za misitu na kusaidia Serikali katika kufikisha ujumbe
chanya kwa wananchi kuhusu uhifadhi.
"Kumekuwepo
jitihada za kuhamasisha Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (USMJ),
hivyo FORVAC imeamua kuja na program hii ili kufanikisha dhana nzima ya
uhifadhi endelevu wa misitu na tunaamini kupitia nyie waandishi
mabadiliko makubwa yatapatikana hivi karibuni kwa kasi," amesema
Msoffe
amesema Tanzania ina zaidi hekta milioni 48.1 za misitu ambapo hekta
milioni 21.6 zipo katika misitu ya vijiji ila takiribani hekta milioni
2.4 ndizo zimehifadhiwa na vijiji. Waandishi wanapaswa kuandika kwa kina
adhari za kukosekana uhifadhi ili Serikali na wadau wengine wajitokeze
kufanya USMJ.
Mratibu
huyo amesema hadi sasa FORVAC imenufaisha zaidi ya watu wadau 330,000
katika Kongani za Lindi, Ruvuma na Tanga na kwamba matamanio yao ni
watu wengi kufikiwa.
"FORVAC
ina malengo ya kuongeza thamani ya mnyororo wa kwenye mazao ya misitu
kama mbao, mkaa asali na mengine yanayopatikana msituni huku misitu
ikiwa endelevu," amesema.
Mshauri
wa kiufundi wa FORVAC, Tanzania Juhani Härkönen amesema wanaridhishwa
na mafanikio yanayopatikana katika wilaya 12 zilizopo kwenye program
hiyo inayotarajiwa kuisha 2022.
Ametaja
baadhi ya Wilaya hizo kuwa ni Handeni Kilindi, Kiteto na Mpwapwa,
Ruangwa, Nachingwea, Liwale, Tunduru Namtumbo, Mbinga, na Nyasa,
Mpwapwa, Handeni na Kilindi.
"Tunaamini
FORVAC itachochea USMJ ila watu wa kuonesha matokeo chanya au hasi
katika program hii ni nyinyi waandishi, na sisi tumedhamiria kuchochea
mabadiliko hayo," amesema.
Kwa
upande wake Ofisa Maliasili wa Mkoa wa Lindi Zawadi Jilala , amesema
mkoa unaungana na FORVAC pamoja na taasisi nyingine ambazo zimejikita
kwenye uhifadhi wa misitu kwa njia endelevu.
Amesema
mkoa huo unazaidi ya hekta 900,000 za misitu ambayo ipo kwenye vijiji
70 hivyo ili kuifanya iwe endelevu wanahitajika wadau mbalimbali
kushirikiana nao.
Joseph amesema mafanikio mengine ambayo yamepatikana kupitia miradi ya USMJ ni pamoja na mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Wakufunzoi
Sianga na Mfugale waliwataka waandishi hao zaidi ya 23 kujikita kwenye
uandishi wa kiuchunguzi wa misitu ili waweze kuibua mambo mazuri na
mabaya yanatokea hasa katika sekta ya misitu.
Wamesema habari za uchunguzi zinahitaji muda, kujituma, kujiamini na kuweka maslahi ya umma mbele.
"Habari
za uchunguzi zinahitaji kujituma kweli sio lelemama tunaamini hadi
mwisho wa program tutakuwa na asilimia 20 ya wanaofanya habari hizi,"
amesema.
No comments:
Post a Comment