Ofisa Misitu Wilaya ya Liwale, Nassoro Mzui akielezea utekelezaji wa mradi wa USMJ kijiji cha Darajani, Kata ya Mihumo. Kushoto ni Ofisa Sera na Uraghibishaji wa MJUMITA, Elida Fundi.
Wanakijiji wa Darajani wakiwa wanafatilia kwa makini kuhusu USMJ kijijini kwao.
NA SULEIMAN MSUYA, LIWALE
TOFAUTI
za kisiasa, uvunaji haramu wa rasilimali misitu katika Msitu wa
Narungombe zimetanjwa kuwa ndio sababu kubwa ya kijiji cha Darajani
kuchelewa kutekeleza Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii
(USMJ).
Msitu wa Narungombe wenye ukukwa kwa hekta 5,033 ni sehemu ya Msitu wa Angai uliopo wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Taarifa
hizo za kukwama kwa miradi ya USMJ, zimetolewa na wananchi wa kijiji
hicho mbele ya waandishi wa habari za mazingira, uhifadhi na misitu
waliokuwa katika ziara ya kujifunza na kuona mafanikio na changamoto za
usimamizi shirikishi wa misitu vijijini.
Waandishi
hao kutoka vyombo mbalimbali waliambatana na maofisa wa Mtandao wa
Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) na Shirika la Kuhifadhi
Misitu Asili Tanzania (TFCG) ambayo yanatekeleza Mradi wa Kuhifadhi
Misitu kwa Kuwezesha Biashara Endelevu ya Misitu (CoFOREST) chini ya
ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC).
Akizungumzia
kukwama huko kwa miradi ya USMJ, Mzee wa kijiji hicho Abdulrahman
Ngokwe amesema walikataa mradi huo kupitia vikao halali vya kijiji
kutokana na uelewa tofauti na mwingiliano wa kisiasa.
Amesema
katika kipindi hicho Serikali ya kijiji kilikuwa chini ya Chama cha
Wananchi (CUF) ambao amedai kuwa walikuwa wakipinga mambo mazuri.
Mzee
Ngokwe amesema pia walikuwepo watu wachache ambao walikuwa wanavuna kwa
njia haramu hivyo kutumia wingi wao kuwagawanya ili wao waweze
kunufaika.
"Sisi
tumakataa mradi huu kwa sababu za kisiasa na uvunaji haramu hali ambayo
imeturudisha nyuma na sisi kati ya vijiji vinne vya kata ya Mihumo
tumebaki nyuma kimaendeleo," amesema.
Amesema baada ya kupata elimu na kuona manufaa ya majirani zao wa Likombora, Turuki na Mihumo ambao wamefanikiwa.
Zaituni Likwata Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili amesema wamejipanga kusimamia kwa makini ili waweze kumufaika na msitu wao.
Likwata
amesema wanatarajia kupitia Msitu wa Narungombe wanafanikiwa kutekeleza
miradi ya ujenzi wa shule, kupata vitendea kazi vya ulinzi wa misitu.
Aidha, amesema elimu waliyopata imechochea wanawake wengi kushiriki kwenye USMJ.
Mussa Abdallah amesema pamoja na siasa kukwamisha USMJ uelewa ulikuwa mdogo ila sasa wapo vizuri.
"Sisi tulifanya ujinga ila kwa sasa tupo pamoja kushiriki kikamilifu kulinda msitu wetu na kuundeleza," amesema.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Darajani Hamisi Mbanila amesema Serikali ya kijiji ipo
tayari kushiriana na wananchi na serikali yote ili misitu iwe na tija
kwa jamii ya Darajani.
"Elimu imesaidia kila mwanakijiji ni mlinzi wa msitu kwani maendeleo ya vijiji jirani yanawaumiza," amesema.
Ofisa
Misitu wa Wilaya ya Liwale, Nassoro Mzui amesema wilaya yao ina vijiji
27 vyenye misitu ya asili ambapo vijiji 23 vipo ndani ya Msitu wa Angai
na vijiji vinne vipo nje ya Msitu wa Angai.
Amesema USMJ Liwale inatekelezwa na Program ya Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu (FORVAC) na CoFOREST.
Amesema
pamoja na mafanikio ambayo yamepatikana kupitia miradi hiyo bado ipo
changamoto ya ukubwa misitu hivyo ulinzi kuwa hafifu.
Mzui amesema Halmashauri ya Liwale inajivunia kwa kuondoa idadi ya vijiji tegemezi kutoka bajeti ya wilaya.
Amezitaka wilaya nyingine nchini kuhamasisha USMJ kwani ni mfumo rafiki na endelevu kwa misitu ya vijiji.
Ofisa
Sera na Uraghibishaji kutoka MJUMITA amesema wameamua kuzunguka na
waandishi ili waone na kujifunza faida zilizopo kwenye USMJ.
"Vijiji
vinanufaika sana kiuchumi, kimaendeleo, kijamii huku uhifadhi ukiwa
mzuri tofauti na vijiji ambavyo havina USMJ," amesema.
Fundi
ameziomba taasisi mbalimbali kwenda kwenye vijiji ambao vina misitu ya
asili na kusambaza elimu ya USMJ ili kuweza kuokoa zaidi ya hekta
milioni 17 kati ya milioni 22 za misitu ya vijiji.
Amesema iwapo waandishi wataweka bayana mafanikio ya USMJ watunga Sera na wafanya maamuzi watajua umuhimu wake.
No comments:
Post a Comment