Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge
ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya Mkandarasi wa kampuni ya CICO
anayetekeleza Mradi wa ujezi wa Daraja la Ulongoni "A" ambalo Ujenzi
wake umekuwa ukisuasua jambo linalosababisha usumbufu kwa wakazi wa
Ulongoni.
Kutokana na
hilo RC Kunenge ametoa agizo kwa mkandarasi, mshauri Mradi,mratibu wa
DMDP kufika ofisini kwake Jumatano ya November 25 huku akimuelekeza
meneja wa TANROAD Mkoa kumpatia Mtaalamu wa kufanya ufuatiliaji na
uchunguzi wa utendaji kazi tangu kuanza kwa Mradi huo Hadi sasa.
Aidha
RC Kunenge amesema kitendo Cha uzembe wa mkandarasi huyo ni
uchonganishi baina ya wananchi na Serikali yao ambayo iliahidi kujenga
Daraja hilo na tayari Serikali ilishatoa fedha za Ujenzi huo lakini
mkandarasi amekuwa akikwamisha juhudi hizo.
Hata
hivyo RC Kunenge amepinga sababu zilizotolewa na mkandarasi huyo kuwa
Ujenzi umechelewa sababu ya Corona na Mvua wakati miradi kwenye maeneo
mengine inaendelea Kama kawaida akitolea mfano wa Ujenzi wa Daraja la
Tanzanite linalopita katikati ya bahari.
No comments:
Post a Comment