HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 23, 2020

TOTAL, YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUWATHAMINI ZAIDI WATEJA WAKE

Three The Hard Way  wa Total ambao ni ma Sterling watatu wa vídeo maalum ya Total The Jerusaléma Challenge, wakiongozwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Bw. Jean-Francois Schoepp,  katikati, Meneja Mtandao wa Vituo vya Mafuta vya Total, Network Manager, Mariamme Saw (kulia) na Mkurugenzi wa sheria na mahusiano wa Total, Tanzania, Bi. Marsha Msuya Kileo,  katika hafla ya kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja ya Total kwa mwaka huu wa 2020, katika kituo cha mafuta cha Total Africana, kilichopo êneo la Africana, Mbezi Beach, Dar es Salaam. Wiki hiyo imehitimishwa kwa Total Kurekodi Video maalum ya wimbo huo.


Three The Hard Way  wa Total ambao ni ma Sterling watatu wa vídeo maalum ya Total The Jerusaléma Challenge, wakiongozwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Bw. Jean-Francois Schoepp,  katikati, Meneja Mtandao wa Vituo vya Mafuta vya Total, Network Manager, Mariamme Saw (kulia) na Mkurugenzi wa sheria na mahusiano wa Total, Tanzania, Bi. Marsha Msuya Kileo,  katika hafla ya kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja ya Total kwa mwaka huu wa 2020, katika kituo cha mafuta cha Total Africana, kilichopo êneo la Africana, Mbezi Beach, Dar es Salaam. Wiki hiyo imehitimishwa kwa Total Kurekodi Video maalum ya wimbo huo.


Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Bw. Jean-Francois Schoepp,  katikati, Meneja Mtandao wa Vituo vya Mafuta vya Total, Network Manager, Mariamme Saw (kulia) na Mkurugenzi wa sheria na mahusiano wa Total, Tanzania, Bi. Marsha Msuya Kileo,  wakiselebuka  ndani ya moja ya maduka ya Bonjour yaliyopo kwenye kila kituo cha Total, katika hafla ya kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja ya Total kwa mwaka huu wa 2020, katika kituo cha mafuta cha Total Africana, kilichopo êneo la Africana, Mbezi Beach, Dar es Salaam. Wiki hiyo imehitimishwa kwa Total Kurekodi Video maalum ya wimbo wa The Jerusaléma Challenge.


Wafanyakazi wa Total Tanzania katika picha ya ku pose na bidhaa za vilainishi vya Total, wakati wa hafla ya kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja ya Total kwa mwaka huu wa 2020, katika kituo cha mafuta cha Total Africana, kilichopo êneo la Africana, Mbezi Beach, Dar es Salaam. Wiki hiyo imehitimishwa kwa Total Kurekodi Video maalum ya wimbo wa The Jerusaléma Challenge.  

Wafanyakazi wa Total Tanzania, katika picha ya pamoja na  Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Bw. Jean-Francois Schoepp, ( katikati mwenye kofia nyekundu)  wakati wa kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja ya Total kwa mwaka huu wa 2020, katika kituo cha mafuta cha Total Africana, kilichopo êneo la Africana, Mbezi Beach, Dar es Salaam. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu  ni  “Kwa Total, mteja ni zaidi ya mteja, ni mshirika”. Maadhimisho hayo yameadhinishwa kwa wiki nzima kwa shughuli mbalimbali na kuhimishwa leo kwa kurekodi Video maalum ya wimbo wa The Jerusaléma Challenge.
 

 

Na Mwandishi Wetu 

 

Kampuni ya mafuta ya Total, ambayo ndio kampuni inayoongoza kwenye uuzaji na usambazaji wa mafuta nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 50, imehitimisha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kwa kuwathamini zaidi wateja wake kuwa ni zaidi ya wateja, sasa inawaita ni washirika wa Total, na katika kufunga mwaka, inawaandalia zawadi maalumu ya kufungia mwaka ambayo itatolewa hivi karibuni, japo haikutajwa itakuwa ni zawadi gani. 

 

Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha wiki hiyo ya huduma kwa wateja ya Total, Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Bw. Jean-Francois Schoepp alisema, “Total tunaamini na kutambua kuwa wateja wetu ni zaidi ya wateja, ni washirika wetu.  Wao ndio chanzo cha biashara na mafanikio ya Total nchini. Tunawashukuru sana kwa kuendelea kutuunga mkono na kutuamini. Tunawakaribisha wote kutupa mawazo na maoni yenu juu ya huduma zetu ili tupate kuziboresha na kuwapa huduma  bora  zaidi.”

 

 

Aidha aliongeza kuwa, Total imekuwa ya mafanikio makubwa sana kutokana na jitihada za wafanyakazi wa Total na kuwashukuru wafanyakazi wa Total kwa kujituma katika kuhakikisha kuwa Total imekuwa ya mafanikio. 

 

 

Kwa upande wake, Mkufunzi wa Vituo vya Total, Msafiri Josephat Shigella, amesema lengo la maadhimishoya wiki ya mteja ni kutoa fursa kwa uongozi na menejmenti ya Total, kukutana ana kwa ana na wateja, kuwasikiliza na kujua mahitaji yao. 

 

 

Mkurugenzi wa Mtandao wa vituo vya mafuta vya Total, Marriame Saw, amewashukuru sana wateja wa Total kwa kuichagua Total na kuahidi kuendelea kupanua mtandao wa vituo vya mafuta vya Total ambayo kwa sasa, tayari wanavyo vituo zaidi ya 100.

 

 

Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Total. Marsha Msuya Kileo, ameendelea kuwasisitiza watumia wa mafuta, waendelee kutumia mafuta ya Total,yenye kiambata cha excellium, ili kufaidi mafuta na vilaini na huduma zenye ubora wa hali ya juu.

 

 

Kwa upande wa wateja, wateja waliohojiwa, wamesema mafuta ya vituo vya Total yana tofauti fulani na mafuta mengine yote, ila pia vituo vya Total, vina muonekano fulani unaokufanya wewe dereva kujisikia vizuri kujaza mafuta Total, pia unahudumiwa vizuri.

No comments:

Post a Comment

Pages