December 12, 2020

UTT AMIS YAFUNGUA KITUO CHA KUHUDUMIA WAWEKEZAJI JIJINI MWANZA


Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Kampuni ya Uwekezaji wa Pamoja ya UTT AMIS imefungua kituo cha kuhudumia wawekezaji jijini Mwanza ili kutimiza azma ya Serikali ya kuendelea kuwahudumia wawekezaji karibu zaidi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Uendeshaji na Maendeleo ya Biashara wa UTT AMIS, Issa Wahichinenda alisema kuwa kupitia kituo hicho wanategemea wateja wao kupata huduma mbalimbali ikiwemo ushauri, elimu ya uwekezaji kwenye mifuko ambayo wanaiendesha, kufungua akaunti, kuuza na kununua vipande, kupata taarifa za uwekezaji pamoja na kujua thamani ya vipande katika mifuko na huduma nyingine katika uwekezaji.  

Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Tutuba ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa kituo hicho alisema kuwa ni fursa nzuri kwa wale wanaopata fedha kidogokidogo wanaweza wakawekeza na pia wale wanaopata fedha nyingi kwa pamoja wanaweza wakawekeza.


“unatumia faida wakati kiwango cha mtaji kiko palepale, niendelee kuwasihi na kuwahasa wananchi wa mkoa wa Mwanza na watanzania kwa ujumla tujitokeza kwa wingi kuwekeza kwenye mfuko huu wa UTT". alisema Tutubahui.

Kampuni ya UTT AMIS imeanzisha na kusimamia mifuko sita ya uwekezaji wa pamoja nchini yenye mali zenye thamani ya shilingi bilio 412.

 Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Tutubahui, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha kuwahudumia wawekezaji cha Kampuni ya Uwekezaji wa Pamoja UTT AMIS jijini Mwanza. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Maendeleo ya Biashara wa UTT AMIS, Issa Wahichinenda.

Mkurugenzi wa Uendeshaji na Maendeleo ya Biashara wa UTT AMIS, Issa Wahichinenda (katikati), akitoa maelezo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Tutubahui, mara baada ya kuzindua kituo cha kuhudumia wawekezaji jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Pages