HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 04, 2020

WAHITIMU 408 WATUNUKIWA SHAHADA ZA UMAHIRI KATIKA FANI MBALIMBALI CHUO KIKUU MZUMBE KAMPASI YA DAR ES SALAAM

Na Mwandishi Maalum

IDADI ya Wahitimu Wanawake katika Shahada za Umahiri (Masters) imezidi kuongezeka  kwa mara ya tatu mfululizo Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es Salaam, huku Wanawake hao pia wakiongoza katika ufaulu wa masomo katika fani mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho.

Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka wakati akizungumza wakati wa mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam yaliyofanyika leo Desemba 4, 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo. 

 Amesema Katika Ndaki ya Dar es Salaam kwa mwaka wa masomo 2019/20, jumla ya wahitimu 408 wamefuzu masomo yao kwa ngazi ya Shahada za Umahiri katika fani mbalimbali za kitaaluma na wametunukiwa stahiki zao leo.

Amesema kuwa Kati ya wahitimu hao, wanaume ni 198 ni sawa na asilimia 48.5 na wanawake ni 210 sawa na asilimia 51.5 takwimu hizi zinaonyesha katika miaka mitatu mfululizo Ndaki ya Dar es Salaam imekuwa na ongezeko kubwa la wahitimu wanawake kwa kulinganisha na idadi ya wahitimu wanaume. 

Waliotunukiwa stahiki zao leo katika fani mbalimbali ambazo ni Shahada ya Umahili (Masters) ya Uongozi wa Biashara katika menejimenti ya mashirika, Shahada ya Umahili ya Sayansi katika Uhasiu na Fedha, Shahada ya Umahili ya sayansi katika Manunuzi na Ugavi, Shahada ya Umahili ya Sayansi katika Menejimenti na masoko, Shahada ya Umahili ya uongozi wa Biashara katika menejimenti ya mashirika- watendaji wakuu,

Shahada ya Umahili ya ya Sayansi katika Uchumi Tumizi na Baishara, Shahada ya Umahili ya Sayansi katika Menejiment ya Rasilimali watu, Shahada ya Umahili ya Utawala wa Umma, Shahada ya Umahili ya Utawala wa Umma-watendaji wakuu na Shahada ya Umahili ya Uongozi na menejimenti.

Katika Mafali hayo watunukiwa mbalimbali walioongoza katika masomo kwa kupata alama za juu zaidi kuliko wengine wote katika kila fani walipata zawadi ya cheti pamoja na fedha taslimu huku wahadhiri nao waliochapisha maandiko mbalimbali ya taaluma na jamii wakitunukiwa zawadi na Mkuu wa Chuo Jaji Mstaafu, Barnabas Samatta.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Mteule, Rais Mstaafu wa Awamu ya Saba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein amewapongeza wahitimu waliotunukiwa shahada za umahili katika chuo hicho.

Dkt. Shein amesema kuwa atakapo kabidhiwa ofisi hatasita kuomba ushauri kwa Mkuu wa wa Chuo Kikuu Mzumbe Jaji Mstaafu Barnabas Samatta kwani yeye ndio mtangulizi wake katika kuongoza chuo hicho kwani ni kwaajili ya maendeleo ya sekta ya elimu na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

"Nitakapoanza kuongoza Chuo Kikuu Mzumbe najua nitapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wafanyakazi wote wa chuo Kikuu hiki." Amesema Dkt. Shein wakati akitambulishwa kuwa ndiye Mkuu wa Chuo Kiku Mzumbe mpya baada ya Mkuu wa Chuo hicho Mstaafu Jaji Barnabas Samatta kustaafu. 

Hata hivyo Chuo kikuu Mzumbe kimeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu kwa Kampasi ya Dar es Salaam.

Chuo kimekamilisha ukarabati, ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya iliyokuwa Shule ya Sekondari ya Tegeta. Ukarabati na uboreshaji huu ulihusisha kumbi za mihadhara, madarasa, maktaba, maabara ya kompyuta na ofisi za wafanyakazi. 

Kukamilika kwa ukarabati huu kumewezesha kuanza kwa Programu za masomo kwa Shahada za Awali mwezi Novemba, 2020 baada ya kupata kibali kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). Uwezo wa Tawi hili ni kuchukua wanafunzi 1500 kwa mara moja.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka akizungumza katika Mafali ya 19 yaliyofanyika leo Desemba 4, 2020 katika 
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mstaafu Barnabas Samatta akimpongeza, Elieshi Oberlin aliyefanya vizuri katika kozi ya Master of Business Administration in Cooperate Management katika Mahafali ya 19 yaliyofanyika leo Desemba 4, 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Awali (Masters) wakisikiliza kwa makini kinachoendelea katika mahafali ya 19 ya chuo Kikuu Mzumbe yaliyofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mstaafu Barnabas Samatta akimpongeza Mkuu wa Ndaki ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi  leo Desemba 4,2020 katika mahafali ya 19 yaliyofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, baada ya Kuandika machapisho mbalimbali.

Baadhi ya wahadhiri wa Chuo kikuu Mzume katika Mafali ya 19 yaliyofanyika leo Desemba 4, 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Meza Kuu.

Baadhi ya wahitimu katika Mahafali ya 19 yaliyofanyika leo Desemba 4, 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages