HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 12, 2021

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR ASISITIZA UMOJA NA MSHIKANO KATIKA IDARA ZOTE ZA OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameendelea kuhuubiri umoja na  mshikamano katika Nchi ya Zanzibar kwa muda mrefu sasa, na leo ilikuwa ni zamu ya watendaji wake wa Idara kutoka Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Maalim ameyasema hayo aliporipoti rasmi katika Ofisi yake iliyopo Migombani Mkoa wa Mjini Magharib Unguja leo tarehe 11/01/2021.

Maalim Seif amepokelewa na Watendaji wa Ofisi hio wakiongozwa na Kaimu Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Dr. Khalid Salum Mohammed.

Baada ya kuwasili na kukagua maeneo yote ya Ofisi Makamu wa kwanza wa Rais alipata fursa ya kukutana na kuzungumza na Wakuu wa Idara mbali mbali zilizopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.

Katika nasaha zake kwa wakuu wa Idara hao Maalim Seif amewataka Watendaji  wote wa Ofisi hio kuwa nadhifu kuanzia mavazi mpaka maeneo yao ya kazi kwani Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ni miongoni mwa Ofisi kubwa katika Serikali, na muonekano wake pamoja na utendaji mzuri wa kazi unatakiwa kuwa mfano bora.

Maalim Seif pia amesisitiza uwepo wa nidhamu na uwajibikaji  kwa kusema;
”Suala la nidhamu ni suala muhimu sana kwani bila nidhamu hatuwezi kufanya mambo yetu tukapata mafanikio, na Wakuu wa idara musimuonee mtu muhali katika hili na kama mtu asipokuwa na nidhamu aadhibiwe kwamujibu wa sheria ila nasisitiza zaidi asionewe mtu’’.

Sambamba na hilo Maalim Seif amesema  Suala la Mashirikiano ni miongoni mwa jambo la muhimu sana,  na ushirikiano huu uwepo kwa mtu mmoja mmoja lakini pia kwa taasisi kwa ujumla,  na katika kusisitiza hilo Maalim amesema yeye anawakaribisha watendaji wote katika ofisi yake kwa ushauri na ufafanuzi kwa maslahi mapana ya taasisi na Taifa kwa ujumla

Jambo la mwisho  Maalim Seif amezungumzia suala la kujiwekea malengo kama taasisi kwa kuwaambia watendaji yakwamba;

”Tunahitaji tukamilishe majukumu yetu yote yanayotupasa kufanya tena kwa ufanisi mkubwa,  na hili litafanikiwa kama tutajiwekea malengo katika utendaji wetu, niwaombe Wakuu wa Idara na watendaji wote muwe na mikakati ya malengo yetu ya muda mfupi na ya muda mrefu ili kuhakikisha hakuna kitu tutakachokiwacha nyuma’’.

Kwakumalizia Maalim amewaambia Wakuu wa Idara zote zilizopo chini ya Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais kwamba ataanza Ziara Rasmi ya kupitia Idara hizo kuanzia siku ya Jumaatano ili kujua Changamoto na kubadilishana mawazo.

No comments:

Post a Comment

Pages