Na Lydia Lugakila, Muleba
Halimashauri ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera imegawa madawati 836 katika shule za msingi zipatazo 26 kupitia mapato yake ya ndani ambayo yamesaidia kuondoa changamoto ya uhaba wa madawati shuleni.
Akigawa madawati hayo Mkurugenzi Mtendaji wa halimashauri ya Wilaya ya Muleba Bwana Emmanuel Sherembi amesema katika mwaka huu wa fedha halmashauri hiyo ilikuwa na mahitaji ya madawati 51,534 na kulikuwa na madawati 49,576 upungufu ukiwa ukiwa ni madawati 1948.
sherembi amesema kuwa halmashauri ya Wilaya ya Muleba kupitia mapato yake ya ndani imetengeneza madawati 1,036 katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza madawati 200 yalitengenezwa na kusambazwa katika shule za msingi tisa.
Aidha Mkurugenzi huyo ameagiza walimu wakuu kuhakikisha wanakarabati madawati yote ndani ya siku saba kwani ofisi ya Mkurugenzi imetoa kibali cha utengenezaji wa madawati mabovu katika shule zilizoomba 58 ikiwa ni jumla ya madawati 1074 na hivyo kiumaliza kabisa changamoto ya madwati katika Wilaya hiyo.
Awali akisoma taarifa kaimu afisa elimu msingi Wilaya ya Muleba Bi. Restuta Stephano amesema Wilaya ya Muleba ina jumla ya shule za msingi 241 ambapo shule 227 ni za serikali na shule 14 ni shule binafsi jumla yake wakiwa wanafunzi 154,604.
Kwa niaba ya wakuu wa shule wilaya ya Muleba kwa dhati ya mioyo tunatoa shukurani na pongezi za dhati kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Muleba @DC Mlb Eng. Richard Ruyango na Mkurugenzi Mtendaji @Emmanuel Shirembi kwa kutatua changamoto ya madawati katika wilaya yetu.
ReplyDeleteTunawapongeza kwa kazi nzuri iliyotukuka na zaidi tunawaahidi utumishi uliotukuka katika kuhakikisha tunaipandisha wilaya ya Muleba na mkoa wa Kagera juu kielimu👏👏
*James V. Tarimo _(Mjoli wa Bwana)_*
Mkuu wa Shule - Kyota