HABARI MSETO (HEADER)


February 18, 2021

BASHE ATUA SIKU 14 mfuko wa pembejeo kumuandikia mchanganuo wa kiasi cha madeni ya mikopo

 


NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA

NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe, ametoa siku 14 kwa mfuko wa pembejeo nchini kumwandika mchanganuo wa kiasi cha madeni ya mikopo iliyolipwa na wanayodaiwa wakulima ili kuanza kuchukua hatua za ufuatiliaji kwa kuhusisha mamlaka za juu.

Bashe, ametoa maagizo hayo jana jijini Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na watumishi pamoja na viongozi wa mfuko huo.

Amesema, mfuko huo unatakiwa kuweka nguvu katika ukusanyaji wa madeni ya mikopo ambayo wamekopesha wakulima kwakua ni kiasi kikubwa cha fedha mbacho kipo nje.

"Hivyo nauagiza Mfuko wa Pembejeo nchini kuitumia taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Tanzania (TAKUKURU) kudai madeni ya mikopo waliyo wakopesha wakulima kiasi cha Sh. bilini 30,"amesema Naibu waziri Bashe.

na kuongeza kuwa “Kipaumbele chenu kwa sasa lazima kiwe ni kukusanya madeni ya mikopo mliyowakopesha wakulima toka mfuko huu uanzishwe mwaka 1995 ni takribani bilioni 30 zipo nje na kiasi ambacho mmefanikiwa kukusanya hadi hivi sasa ni bilioni 10 pekee”alisema

Aidha amesema kuwa kutokana na hali hiyo mfuko huo unatakiwa kuitumia Takukuru kudai madeni hayo kwa wakulima ambayo yamekuwa ya muda mrefu.

“Nawaomba mwandikie Mkurugenzi wa Takukuru Brigedia jenerali John Mbungo ili muwatumie Takukuru kudai fedha hizi kwani wao wako vizuri katika kudai madeni hawa wengine mtasumbuana tuu na mambo ya mahakamani”alisema Bashe

Pia, Bashe ameuagiza mfuko huo kusitisha utoaji wa mikopo hadia hapo utakapofanya marekebishio ya muundo wake.

“Mfuko huu toka uanzishwe mwaka 1995 haujawahi kutengeza faida na hii ni ktokana na muundo wenu mnatoa mikopo lakini mlivyo kama siyo taasisi inayojihusisha na utoajiwa fedha”amesema Bashe

Vile vile, amesema kuwa moja ya sababu inayochangia kiasi kikubwa cha fedha kupotea kutokana na mikopo chechefu ni kwasababu ya kukosekana kwa bima ya mikopo.

“Kutokuwepo kwa bima ya mikopo kunasabaisha sana fedha kupotea kutokana wakulima wakati mwingine kushindwa kurejesha kutokana na mabadiliko tabia ya nchi na majanaga mbalimbali hivyo kabla hamjaanza kutoa mikipo mingine muhakikishe kwanza mnakuwa na bima ya mikipo”alisema

Kadhalika, Bashe aliutaka mfuko huo kuvunja mikataba yote waliyoingia na makampuni binafsi ya kudai madei hayo kwa wakulima.

Mkurugenzi mtendaji wa mfuko huo Festo Mhimba, amesema kuwa wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo mabadiliko tabia nchi kama vile mafuriko, ukame hali ambayo inachangia wakulima kushindwa kurejesha mikopo.

“Kikwazo kingine ni wadaiwa kuweka mazuio mahakamani wakati wa kufuatilia madeni kwa kuuza dhamana hali ianyosababisha kuchelewa kwa marejesho kwa kuwa kesi huchukua muda mrefu”amesema Mhimba

Hata hivyo, amesema kikwazo kingine ni dhana potofu iliyopo miongoni mwa wakopaji kuwa fedha ya serikali ni ruzuku hali ambayo hurudisha nyuma hamasa ya urejeshaji.

“Janga la corona pia limesababisha wakopaji kukosa soko la mazao ya kilimo, mifugo nauvuvi kutokana na nchi nyingi kikanda na kimataifa kujifungia”alisema Mhimba.

No comments:

Post a Comment

Pages