HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 18, 2021

RC NDIKILO AMFAGILIA MENEJA WA TANESCO KWA KUPAMBANIA KITUO CHA KUPOOZEA UMEME MLANDIZI KIFANYE KAZI

 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wa kati kati akizungumza na baadhi ya watumishi wa Tanesco wakati wa ziara yake ya kikazi ya  siku moja yenye lengo la kutembelea kituo cha kupoozea umemecha mlandizi kilichopo Wilayani Kibaha ambacho kinatarajia kuanza kufanya kazi mwezi machi mwaka huu baada ya kuungua na moto mwaka jana.

Mwonekano wa baadhi ya mitambo ambayo tayari imeshafungwa katika kituo hicho cha kupoozea umeme cha mlandizi kilichopo wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ambacho kimetembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

 

NA VICTOR MASANGU, PWANI

 

SERIKALI mkoani Pwani imesema kwamba Kituo  cha kupoozea umeme kilichopo mlandizi Wilayani Kibaha ambacho kilipatwa na majanga ya kuungua na moto mwezi machi mwaka jana   hatimaye kimefanyiwa matengenezo  na  kinatarajia kuanza kufanya kazi rasmi  mwezi machi 2021  ambapo kitatoa  huduma ya utoaji wa nishati hiyo katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani   ikiwemo  Wilayani za Kibaha pamoja na  Bagamoyo.

 Hayo yalibainishwa  na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya kutembelea na kujionea maendeleo na matengenezo mbali mbali katika kituo hicho ambapo ameupongozeza uongozi wa  Shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani  kuweza kuboresha miundombinu ambayo ilikuwa imeharibika  hapo awali na kuwa kero  kubwa kwa wananchi hao kukosa umeme.

Ndikilo alifafanua kwamba baada ya kutokea kwa janga la moto katika kituo hicho cha umeme mlandizi baadhi ya wananchi kutoka maeneo mbali mbali walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa nishati hiyo ya umeme kutokana na kukatika mara kwa mara lakini kutokana na juhudi ambazo zimefanyika na Tanesco Mkoa wa Pwani kero hiyo sasa inakwenda kumalizika pindi ifikapo mwezi wa tatu mwaka huu.

“Kwa kweli mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Pwani nimefarijika sana na napenda kuchukua fursa hii kulipongeza sana ten asana Shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani kutokana na kuonyesha nia  ya kufanya yale yote ambayo tulikubaliana na kwa kweli kwa upande wangu nipende kusema kwamba nimeridhishwa na ukarabati na ujenzi ambao umefanyika hii ni dalili nzuri katika Mkoa wetu wa Pwani kuwa na nishati ya Uhakika.

 

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani alisema kwamba kwa sasa  mahitaji ya umeme Katika Mkoa  ni yanayohitajika ni mega watt zipatazo 117.8 na kwamba  kukamilika na kuanza kutoa hudua kwa kituo hicho ni moja ya kuleta maendeleo makubwa katika kukuza uchumi pamoja na kuwavutia wawekezaji mbali wa ndani na nje ya nchi.

Kadhalika alizitaka mamlaka nyingine  ikiwemo Dawasa pamoja na Tanrods kuhakikisha kwamba wanaweka mipango endelevu ya kudhumisha huduma zao kwa wananchi ikiwemo kurekebisha miundombinu m bali mbali ya barabra ili iweze kupitika kwa urahisi kuingia kwenye viwanda amabvyo vipo katika Mkoa wa Pwani.

 

“Tanesco leo kwa kweli nimetembelea kituo hiki cha kupozea umeme wamenirufarisha sana kwa kuwa nimejionea mimi mwenyewe kwa jinsi walivyofunga mitambo na laini mbali mb ali ambazo zinatumika katika kuwasambazia umeme wateja mbali mbali wa Wilaya ya Kibaha pamoja na Bagamoyo pamoja na katika maeneo ya viwanda na hi ni hatua kubwa kwa hivyo na taasisi zingine kama Dawawa na Tanrods na wao waige mfano huu wasifanya kazi mezani ila wafanye kwa vitendo kama Tanesco.

 

Ndikilo pamoja na kulipongeza Shirika hilo la Tanesco Mkoa wa Pwani lakini pia amelitaka lifanye jitihada za makusudi katika kpelekeka umeme wa uhakika katika Wilaya ya Mkuranga ambayo nao inauwekezaji mkubwa wa viwanda na kujenga kituo maalumu cha kupozea umemem amabcho kitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuliko kutegemea kwa kiasi kikubwa umeme kutoka katika kituo cha Mbagala kilichopo Jijini Dar es Salaam.

  

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani Mhandisi Mahawa Mkaka amebainisha kwamba kituo hicho mwaka jana kiliweza kuungua na kusababisha hasara kubwa na kusababisha changamoto kubwa ya baadhi ya maeneo   kukatika katika kwa umeme mara kwa mara na kwamba kituo hicho kitakuwa  mkombozi mkubwa kwa wananchi kupata umeme wa uhakika.

Naye Mkuu wa kituo hicho cha kupozea umeme cha mlandizi Baraka Zonga kituo hicho cha kupoozea umeme kina transfoma kubwa nne amabzo zitakuwa na uwezo wa kusambaza umeme katika laini saba katika maeneo mbali mbali ikiwemo katika mitambo ya  maji ya ruvu juu pamoja na ile ya ruvu chini sambamba na maeneo mengine ya viwanda na bandari kavu ya Kwala.

Mkoa wa Pwani kwa sasa imetajwa kuwa kinara katika uwekezaji wa viwanda hivyo kuboresha kwa miundombinu ya umeme na kuanza  kufanya kazi  tena kwa kituo hicho cha kupoozea umeme mlandizi kitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi pamoja na wawekezaji wa viwanda kupata  umeme wa uhakika.

No comments:

Post a Comment

Pages