NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewaongoza wakazi wa Jiji la Dodoma kuuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi kwenye hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) BaloziKijazi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali hiyo Jijini hapa alipokuwa amelazwa kwa matibabu
Akimzungumzia marehemu Kijazi, Profesa Ndalichako amesema alikuwa ni mtu mpole, mnyenyekevu,mtulivu mchapakazi na mzalendo aliyekuwaanafanya kazi yake kwa mujibu wa sheria.
“Kwa waleambao tumefanyakazi kwa karibu na marehemu Balozi Kijazi alikuwa ni mtu wa upendokwa watu wote na pia alikuwa anatutaka tufanyekazi zetu kwa kuzingatiataratibu, kanuni na sheria za utumishi wa umma katika kutekeleza majukumu yetuya kila siku,” amesema Profesa
Ndalichako Ameongezakuwa, “Balozi Kijazi alikuwa anafuatilia utekeleaji wa maazimio yoteyanayofikiwa kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri ili kuhakikisha kuwa kilakilichoazimiwa kinakamilika kwa wakati hakika tumempoteza mtu muhimu sana hapanchini.
"Kwa upandewake Katibu Mkuu Ikulu, Moses Kusiluka alisema ibada ya kiserikali ya kumuaga Balozi Kijazi itafanyika Jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Karimjee ambapo Rais John Magufuli atawaongoza wakazi wa Jiji hilo kuuaga mwili huokabla ya kusafirishwa kwenye nyumbani kwao Wilayani Korogwe mkoani Tanga kwamazishi yatakayofanyika (jumamosi).
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, (UDOM) Profesa Faustine Bee alisema alikuwa anatamani kuendelea kufanya kazi na Balozi Kijazi kwani hata katika changamoto nyingi za chuo hicho walikuwa pamoja katika mapambano ambapo haki ,wajibu na unatawala vilidumu na watanzania kukimbilia chuo hicho kusoma na kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment