Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani
Jafo akikagua machinjio ya kisasa ya Manispaa ya Kigoma ambayo ujenzi
wake umeanza bila kufuata taratibu za kimazingira za kutosajili Mradi
huo kwa ajili ya kupata Cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira.
Waziri Jafo ametoa siku 10 kwa Manispaa hiyo kusajili Mradi huo Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
NA LULU MUSSA, KIGOMA
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo
ametoa siku kumi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma kuhakikisha
anasajili mradi wa ujenzi wa Machinjio ya kisasa ili uweze kupata cheti
cha Tathmini ya Mazingira.
Akiwa
katika siku ya pili ya ziara yake Mkoani Kigoma Waziri Jafo ametembelea
machinjio ya Manispaa ya Kigoma na kubaini ujenzi unaendelea bila
kufuata taratibu za kimazingira kwa kuwa hauna Cheti cha Tathmini ya
Athari ya Mazingira.
"Naagiza
mradi huu usajiliwe mapema iwezekanavyo, na lengo la kufanya hivi si
kupata cheti tu bali muhimu ni kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala
muhimu ya kuzingatia katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira," Jafo
alisisitiza
Waziri Jafo
amesema endapo Manispaa ya Kigoma itashindwa kusajili mradi huo wa
machinjio ya kisasa kwa kipindi tajwa atasitisha ujenzi huo.
"Hivi
sasa kuna mfumo wa kusajili miradi kwa njia ya mtandao na miradi yote
naiona hapa kwenye tablet yangu sasa ikifika tarehe 25/05/2021 sijaona
mradi wenu nitasitisha ujenzi wenu" Jafo alisisitiza.
Pia,
Waziri Jafo amewataka wawekezaji kote nchini kusajili miradi yao ili
iweze kukidhi vigezo vya kupatiwa cheti cha Tathmini ya Athari kwa
Mazingira kinacho ainisha namna bora ya kupunguza madhara ya kimazingira
yatikanayo na utekelezaji wa miradi.
Katika
hatua nyingine Waziri Jafo amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha
inahamasisha wawekezaji kuwekeza katika uzalishaji wa nishati mbadala
ambayo ni rafiki kwa mazingira.
Waziri
Jafo ameyasema hayo mara baada ya kutembelea Mradi wa Nishati ya Jua na
kuridhishwa na uzalishaji rafiki kwa mazingira ambao uzalisha kiasi
Mega Watt 1 kwa sasa huku lengo likiwa ni kuzalisha Mega Watt 4.8
kufikia 2025.
Amesema
umeme unaozalishwa kutoka katika Mini-grid ya Kigoma unafaida kubwa
kimazingira kwa kuwa unapunguza matumizi ya umeme wa Mafuta ambao
gharama yake ni kubwa na kupongeza Uongozi wa Mkoa wa Kigoma kwa kutumia
Green Power
No comments:
Post a Comment