Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye, akitoa hotuba yake wakati wa kufunga Kongamano la
Kimataifa la Kuadhimisha Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania.
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, akifunga Kongamano la Kimataifa la Kuadhimisha Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye (kushoto), akimkabidhi tuzo Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga ya kutambua mchango wa wizara hiyo katika kufanikisha Kongamano la
Kimataifa la Kuadhimisha Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania.
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, akimkabidhi tuzo Prof. Victor Mlekwa (katikati) kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha kongamano hilo.
Mshiriki kutoka Nigeria, Dk. Danlanin Hayyo akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi.
Dk. Titilayo Adeoye Ajadi akipokea cheti kutoka kwa Naibu Waziri.
Dk. Titilayo Adeoye Ajadi akipokea cheti kutoka kwa Naibu Waziri.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Serikali
imekihimiza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taasisi nyingine za elimu
kufanya tafiti zitakazosaidia kutoa machapisho na majarida
yatakayoisaidia kuleta hamasa na msukumo wa jamii kushiriki katika elimu
ya watu wazima ili kusaidia kuendelea kupunguza kundi la watu wasiojua
kusoma, kuhesabu na kuandika pamoja na kuchochea maendeleo endelevu.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga katika Kilele cha Kongamano la
Kimataifa la Kuadhimisha Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania
lililoandaliwa na chuo hicho kupitia Shule Kuu ya Elimu.
Amesema
chuo hicho kwa kushirikiana na taasisi nyingine za elimu kina wajibu wa
kufanya tafiti zitakazosaidia kutatua changamoto zinazoikabili elimu ya
watu wazima kwa kutoa machapisho na majarida yatakayosaidia jamiii
kuondokana na ujinga.
" Nakihimza UDSM na
taasisi za elimu mshirikiane katika utafiti wa elimu hii kisha mchapishe
machapisho na majarida ya kutoa hamasa na kuhimiza jamii ishiriki
katika madarasa ya MEMKWA," amesema Naibu Waziri Kipanga.
Amebainisha
kuwa Serikali iko tayari kushirikiana na chuo hicho kwa kuhakik,isha
elimu hiyo inawafikia watu wote wenye mahitaji nayo hivyo alikiomba UDSM
kuendelea kushirikiana na wadau wa elimu kutatua changamoto
zinazoikabili elimu hiyo.
Ameiomba Tume ya Vyuo
Vikuu Nchini (TCU) kukipatia idhini chuo hicho kuanza kutoa Shahada ya
Uzamili ya Ellimu ya Watu Wazima na kukipongeza kwa kuandaa kongamano
hilo la siku tatu lililojadili mada kuhusu elimu hiyo.
Kwa
upande wake Amidi Mkuu wa Shule hiyo Daktari Eugenia Kafanabo amesema
kongamano hilo lilijadili mada mbalimbali ikiwemo mchango wa Hayati
Mwalimu Julius Nyerere katika kuipigania na kuhamasisha jamii kushiriki
katika kupata elimu hiyo pamoja na kuweka msisitizo wa kufufua madarasa
ya elimu ya watu wazima..
Naye Makamu Mkuu wa
Chuo hicho Profesa William Anangisye amesema chuo hicho kitaekeleza
agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kufanya tafiti kuhusiana na
changamoto na majibu yake kwani katika mwaka wa fedha 2021/22 kimetenga
Sh Bilioni 2 kwa ajili ya tafiti.
Profesa
Anangisye amesema kongamano hilo lmeleta fursa ya wadau wa elimu hiyo
kuwaleta pamoja ambapo walibalishana uwezo na mawazo kwa kujadili mada
mbalimbali za kuendelea kuimarisha utoaji wa elimu hiyo nchini.
Afisa
Elimu ya Watu Wazima kutoka Mkoa wa Mwanza Josephat Sheja amesema
kongamano hilo limetoa maazimio mbalimbali ikiwemo Maafisa elimu mikoa
na wilaya kuboresha madarasa ya MEMKWA kwa kuboresha programu, Serikali
kuangalia uwezekano wa kuifanya elimuhiyo kuwa na idara inayojitegemea
pamoja na wahitimu wenye vyeti, shahada kutambuliwa katika muundo wa
utumishi wa umma.
No comments:
Post a Comment