Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda akipokea zawadi ya kahawa kutoka kwa akina mama wajasiriamali wa kahawa.
Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
WAZIRI wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa bado kuna uhaba wa fedha za kigeni kwa ajili ya kuharakisha Maendeleo ya nchi.
Hayo ameyasema jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa siku maaum ya Kahawa nchini kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, maonesho hayo yalianza Juni 28 na yanatarajia kimalizika Julai 13 Mwaka huu.
Waziri huyo amesema soko la nje ni muhimu hivyo kuna haja ya kuitangaza kahawa ya Tanzania na kwamba inapotengenezwa itengenezwe kwa ubaora kuanzia uvunaji.
Prof. Mkenda amesema watashikamana na bodi ya kahawa kama ilivyo kwa bodi nyingine kwani kuna sehemu wakulima wameshaanza kukata tamaa wanaona hailipi.
Amesema kuwa kilimo kilimwe kwa tija katika sehemu zinazolima ili kuongeza fedha za kigeni na kahawa ina nyweka duniani na itaendelea kunyweka.
" Nampongeza ndugu yangu Amir Hamza kahawa ya Amimza aLtd madukani Nairobi,Kenya inauzawa. Tungependa kuona kahawa yetu ina sheheni kwenye masupamaketi ya Arika Kusini, Angola, Namibia, Botswana, Zimbabwe, Tunisia tuende hadi China, amesema.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania,Prof. Aurelia Kamuzora amesema kuwa kampeni ya unywaji wa kahawa Kuna fuata mnyororo wa thamani mkulima anavutwa na wanywaji kama hawatakuwepo kilimo cha kahawa kitakwama.
"Kunywa kahawa Kuna faida zake na kwa sasa kuna mtandao tafafhali nendeni mkatafute, kuna faida zaidi ya 100 za kinywa kahawa,"amesema Mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa nchi ya Marekani ndio inayofanya mabadiliko mengi ya kidunia na ndio maana wanywaji Kwanza duniani ni nchi hyo.
Amesema kuwa inashauriwa asubuhi kunywa kikombe kimoja cha kahawa ili kuamsha ubongo uweze kufanya kazi vizuri na kwamba nchi za nje wanafanya hivyo lakini nchini walimaji wanakunywa kidogo.
Prof.Kamuzora ameeleza kuwa kunywa kahawa angalau kikombe kimoja kwa siku ili kusaidia ubongo kufanya kazi na kwamba unywaji ukiongezeka mkulima atafaidika.
"Namshukuru waziri wa viwanda na biashara Prof. Mkumbo kwa kufanya mazingira mazuri ya uwekezaji watu wanajitokeza kuchukua leseni za kuanzisha biashara za kahawa,"ameongeza kuwa.
Tafadhali tafuteni leseni ili mfanye biashara tuvute kilimo kwani huwezi kutenganisha biashaa ya kahawa na kilimo " amesema Prof. Kamuzora.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi hiyo
Priscus Kimaryo amesema zao la kahawa linashika nafasi ya pili duniani badala ya maji kwa kunywa.
Amesema kipindi cha nyuma kahawa ilikuwa inazalishwa kwenye nchi zinazoendelea na kutumiwa katika nchi hizo lakini kwa sasa hadi nchi zinazolima nazo zinatumia kahawa.
" Kwa mfano nchi ya Brazili ni ya kwanza kwenye uzalishaji na ni ya pili kwa unywaji wa kahawa duniani ukiachia Marekani, nchi zinazozalishwa zenyewe zina kunywa kahawa kwa Tanzanai utamaduni wa kunywa ulikuwa zaidi kwenye mikoa ya Pwani na visiwani Zanzibar," amesema.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa hivi sasa asilimia kubwa ya unywaji upo kwenye vijiwe na kwamba Tanzania ina viwanda 28 vya kukaanga imetoka kwenye kuacha kukoboa na kwenda kwenye viwanda hivyo.
Amesema pamoja na uwepo wa viwanda hivyo uzalishaji Hali ya unywaji wa kahawa upo chini kwa wastani wa asilimia 7.
" Mkakati uliopo ni kufikia asilimia 15 ya tunachokizalisha, duniani hivi sasa ndio ambayo watu wake wanakunywa kahawa na haina matatizo," amesema.
Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa kuna changamoto kubwa ya za mashine ikilinganishwa ma sekta ya chai mashine zake ni gharama na vifingashio pia.
"Changamoto nyingine ni kwa wale wanaotengeneza kahawa wapo wachache, tunaendelea kutoa elimu kama bodi kuhakikisha wanakuwa wengi " amesema.
Pia amesema mkakati walionao ni kukuza unywaji w kahawa na kuwashauri wawekezaji wa vifungashio wa hapa nchini wawekeza kwenye utengebezaji was vifungashio hivyo kwani vingi vinatoka nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment