Mkuu wa Kitengo cha Habari na Masasiliano kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Roida Andusamile (kushoto), akimkabidhi cheti cha Usajili wa majina mmoja wa watu walifika katika banda lao.
Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
WANANCHI, wametakiwa kutembelea banda la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ili waweze kupata elimu na kuweza kusajili majina, leseni na alama za biashara zao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Brela, Roida Andusamile katika ndani ya Banda lao kwenye maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere yenye kaulimbiu ya ' Uchumi wa Viwanda Ajira kwa Biashara Endelevu'
Amesema kipindi hiki cha Maonyesho hayo ya 45 wana mabanda mawili lengo ni kuhakikisha wanawafikia wananchi wengi zaidi na kwamba hapo awali walikuwa na banda moja tu.
Mkuu huyo wa Kitengo amesema kusajili majina ya kampuni na kurasimisha biashara inakuwa ni rahisi hata kupata mikopo kushindana katika zabuni mbalimbali zinazotangazwa na Serikali.
"Ni kitu muhimu kwa mfanyabiashara kusajili kampuni ili aweze kufanya biashara zake. Pia unatoa leseni za biashara kundi A ambazo zinatambulika kifaifa na kimaifa mfanyabiashara anaweza kufanya biashara kutoka Mkoa mmoja kwenda mwingine, nchi moja kwenda nyingine "amesema.
Ameongeza kuwa hizo ni leseni tofauti na zile zinazotolewa na Halmashauri ambazo hutolewa ndani ya Wilaya na kwamba mfanyabiashara hawezi kufanya Wilaya nyingine.
Andusamile amesema kuwa Brela ina mtazamo ndio maana wanatoa leseni hizo za kundi hilo na kwamba wanatoa leseni za viwanda.
Mkuu huyo wa Kitengo amefafanua kuwa wafanyabiashara wenye viwanda wanatakiwa kupata leseni kutoka brela hivyo wanakaribishwa ili waweze kupata huduma hiyo.
"Pia tunatoa hatadha kwa wavumbuzi wa vitu mbalimbali kwa anayetaka atambulike kama yeye ndiye mvumbuzi tunatoa hizi hatadha," amesema.
Amesema kuwa mtu anapokuwa amevunbua kitu fulani atapata haki miliki yake ya msingi kutoka brela.
Aidha amewashauri wananchi kusajili alama za biashara kwani Kuna umuhinu wa kufanya hivyo hata ikitokea mtu ameiga alama yake inakuwa nibrahisi kumshitaki.
"Tunawasihi wananchi watumie brela kwani hata gharama za Usajili ni za kawaida ambapo mtu anaweza kuzimudu kwa wenye kampuni inaanzia 90,000 hadi 450, 000 na inategemea na mtaji," ameeleza.
No comments:
Post a Comment