Mkurugenzi wa kampuni ya Amimza LTD, Jibraan Amir Hamza akizungumza na waandishi wa habari
Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa Kampuni ya Kahawa ya Amimza LTD, Jibraan Amir Hamza amesema kuwa Kampuni hiyo inazalisha tani 6000 ambapo kutokana na uzalishaji huo soko la kahawa linazidi kupanda ndani ya nchi na nchi za ulaya.
Pia amesema kuwa hivi sasa hamasa na unywaji wa kahawa umekuwa mkubwa sana ukilinganisha na huko nyuma ambapo jamii hususani watanzania wengi wao walikuwa wanafikiria tofauti kuhusu kahawa.
Akizungumza katika siku ya kahawa dunia kupitia maonyesho ya 45 ya kimataifa ya sabasaba inayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu nyerere barabara ya kilwa wilayani temeke.Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam.Mkurugenzi huyo Amesema kuwa watu sasa wanapenda kunywa kahawa.
Amesema kuwa awali kulikuwepo na fikra jana potofu imejengeka kwamba kahawa inaleta magonjwa ikiwamo shinikizo la damu pamoja na magonjwa ya moyo.Jambo ambalo sio sahihi.
Amesema kuwa kahawa inasaidia mambo mengi katika mwili na pia inaleta nguvu na kumchangamusha mtu na kwa hivyo kupitia siku ya kahawa duniani inatoa fursa ya kuwapatia watu elimu na kusaidia kukuza soko.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo Amesema kuwa nje ya Tanzania kahawa soko lake ni kubwa.
" Kahawa inazalishwa Tanzania halafu hatunywi tunazalisha na kwenda kuuza nje ya nchi hivyo thamani ya kahawa yetu inapungua,"
Na kuongeza."Unapozalisha kahawa na kuitengeneza mwisho wa siku inaleta tija amesema Hamza.
Amefafanua kuwa soko la kahawa ndani ya nchi halipo vizuri sana na sio kubwa lakini kwa sasa Watanzania wameshaanza kupata hamasa ya kunywa kahawa hiyo.
Mkurugenzi huyo amesema kwa sasa vijana wadogo wengi wanakimbilia kahawa tofauti na zamani watu wanataka kuancha kunywa soda na badala yake wajikite unywaji wa kahawa.
Pia ametoa wito kuwa Watanzania wawe na mazoea ya kunywa kahawa na kuanchana na dhana ya kwamba inaleta maradhi.
No comments:
Post a Comment