September 18, 2021

Dkt. Tax afunga mafunzo ya siku tano ya Diplomasia ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, awahaimiza wanakamati kuyatumia kuimarisha uchumi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Zungu akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Stargomena Tax akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku ya tano ya kamati hiyo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa JNICC.


Waziri wa Ulinzi wa Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stargomena Tax akiwa katika pich aya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo mara baada ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

 

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stargomena Tax amefunga Mafunzo ya Siku Tano ya Diplomasia ya  Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama huku akibainisha kuwa wajumbe wa kamati hiyo kuyatumia kuimarisha diplomasia ya uchumi na kulinda maslahi ya nchi.

Ameyasema hayo leo jiijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo hayo kwa wajumbe wa kamati  hiyo yaliyofanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC).

Amesema kuwa mafunzo waliyopatiwa wajumbe ni maalum kwa kuendeleza uchumi wa nchi na kwamba yatawaongezea maarifa katika masuala ya kulinda asilahi ya kijamii na kiusalama hivyo yana tija kubwa kwa taifa.

" Mafunzo hayo ni muhimu kuendeleza  uchumi wa nchi kwani diplomasia inategmea  ulinzi na usalama  nina imani mtayatumia kutetea masilahi mapana ya nchi na kuchochea maendeleo ya uchumi," amaesma Dkt. Tax.

Amebainisha kuwa kamati hiyo ina jukumu la kuhimiza matumizi ya sahaihi ya mitandao na teknolojia kwa ajili ya kuleta maendeleo  kwani isipotumika vyema inawaeza kuhatarisha amani na usalama wa nchi.

Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumteua waziri wa wizara na kwamba atatekeleza majukumu yake kwa weledi na kuzingatia sheria n taratibu zilizowekwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano w Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine amesema mafunzo yalilenga kuwajengea uwezo wajumbe katika masuala ya diplomasia ya uchumi, usalama wa nyaraka za ubalozi na kwamba wabunge wamaejadili na kutoa mapendekezo kwa wizara.

Nae, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Zungu amemuomba katibu wa wizara hiyo kuongeza maafasa biashara kwenye balozi au kufungua vituo vya biashara katika balozi wanazoziwakilisha

Amempongeza Rais Samia  kwa namna anavyoshughulikia masuala ya nchi ikiwemo dhamira yake ya dhati kuifikisha nchi kati ka uchumi wa juu wa kati.

Amefafanua kuwa nchi haiwezi kukwepa kushirikiana na mataifa ya nje katika uwekezaji na miradi ya kimkakati kwani inasaidia nchi kupata teknolojia mpya na ubunifu.

No comments:

Post a Comment

Pages