MUIGIZAJI
maarufu wa Bongo Movie Jackline Wolper amevunja ukimya kwa kueleza
kwamba mtu yoyote ambaye atamchafua,kumdhalilisha au kumkashifu mtoto
wake Pascal a.k a P atamchukulia hatua za kisheria.
Wolper
mwenye weupe na uzuri wake ulioambana na umbo lenye kuvutia ,amevunja
ukimya huo leo Septemba 16, 2021 ambapo ameweka wazi hawezi kumjibu kila
mtu mtandaoni ,hivyo sheria itachukua mkondo wake.
"Siwezi
kumjibu kila mtu atakayekuwa akimdhihaki mtoto wangu bali nitatumia
sheria zaidi na kwa sasa watu wawili wa mitandaoni kurasa za udaku
nimewafikisha katika sheria ndio sababu ya kutoona picha zangu za
ujauzito hazisambazwi zikiwa na matangazo ya kuhusu tiba za
afya,"amesema.
Akipiga
stori zaidi Wolper ametumia nafasi hiyo kueleza sababu za
kutomuonyesha kwa muda mrefu katika Mitandao ya kijamii kama
ilivozoeleka kwa mastaa pamoja na watu mbalimbali mara baada ya
kujifungua.
Wolper
ambaye amepewa ubalozi katika duka la nguo Sweetrolah amesema hivi
;"Niliingia mkataba na Kampuni ya Sweetrolah tangu nilivyokua na
ujauzito wa miezi tisa, nikaona niwe wa kipekee kabisa nisisambaze picha
za mtoto mahali popote pale."
Amefafanua
kuwa ubalozi wa P atautumia kama nafasi pekee ya kutangaza nguo na vitu
mbalimbali vitakavyokua vinapatikana dukani hapo."Wakati tunasaini
mkataba wa ubalozi niliomba vitu vitatu ikiwemo mashabiki zangu kupata
vitu katika duka hilo ambavyo vitakua rahisi kumudu kununua, hivyo
nashukuru kwa kufanikishiwa hilo."
September 18, 2021
Wolper kuwachukulia hatua wanaomsema vibaya mtoto wake mtandaoni, apata ubalozi Kampuni ya Sweetrolah
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment