Na John Marwa
KAMPUNI ya Emirates Aluminum kupitia bidhaa yao mpya ya Emirates Aluminum 'Aluminum Composite Panel' (ACP) wamesaini kandarasi ya miaka 2 kuidhamini Klabu ya Simba katika Tuzo ya Mwezi za Mashabiki.
Zoezi hilo limefanyika Leo makao Makuu ya Emirates Aluminum Sinza Jijini Dar es Salaam ambapo Mtendaji Mkuu wa Emirates Aluminum Deogratius Malandu na Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba Barbra Gonzalez wamesaini kandarasi hiyo mbele ya vyombo vya habari.
Akizungumza kabla ya kusaini mkataba huo Mtendaji Mkuu wa Emirates Aluminum Deogratius Malandu amesema wameamua kuingia kandarasi hiyo mara baada ya kuona manufaa makubwa ya kushirikiana na Klabu ya Simba msimu uliopita.
"Ni furaha Leo kampuni yetu kusaini mkataba wa miaka miwili na Mabingwa wa Nchi Simba SC, tunaamini kushirikiana na Mabingwa kutatufanya na sisi kuwa Mabingwa katika kazi zetu.
"Msimu uliopita tulipata nafasi ya kufanya kazi na Simba na kama taasisi tumeona manufaa makubwa ya kushirikiana na Simba kwani kwa ukubwa wao kuna mahala wametufikisha.
"Sasa tumeamua kuingia mkataba mpya wa miaka miwili wenye thamani ya TSH Milioni 300." Amesema Malandu.
Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba Barbra Gonzalez amewashukuru Emirates kwa utayari wao wa kuendelea kufanya kazi na Simba kwa miaka miwili ama misimu ijayo.
"Ninayo furaha kubwa leo kuwakaribisha ndugu zetu wa Emirates Aluminum ACP katika familia ya Simba SC. Msimu uliopita tulikuwa nao na uzoefu walioupata wameona manufaa makubwa kuendelea kufanya kazi na Simba SC.
"Ni jambo la kupongezwa kwani unapokuwa na motisha kwa wachezaji ama Mfanyakazi inaongeza hamasa ya ufanyaji kazi na ushindani wenye faida kwa taasisi husika.
"Sisi kama Simba tunashukuru sana kwani Tuzo hii imekuwa ikiwaongezea Wachezaji wetu hamasa nankujitimu zaidi jambo linalooelekea timu yetu kufanya vizuri." Amesema Barbra n kuongeza kuwa.
"Mkataba huu ni wa miaka miwili wenye thamani ya TSH Milioni 300, tunaamini utaenda kuongeza thamani zaidi kwa wachezaji wetu na Klabu Kwa ujumla. Amesema
Emirates Aluminum ACP itakuwa sehemu ya Klabu ya Simba kwa miaka miwili ijayo ambapo itakuwa inatoa tuzo ya mchezaji bora wa mwezI lakini pia ikiambatana na Tuzo ya Msimu kwa wachezaji waliofanya vizuri zaidi n kuchaguliwa na mashabiki.
No comments:
Post a Comment