Wanataaluma wa Chuo Kikuu Mzumbe na UDSM wakiwa katika maandamano wakati mwili ukiwasili katika ukumbi wa Nkrumah.
Wanataaluma kutoka Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu Dar es Salaam wakiwa katika maandamano Kuelekea Ukumbi wa Nkruma baada ya kupokea mwili wa marehemu Prof. Matthew Luhanga
Viongozi mbalimbali wa taasisi wakiomgozwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Dkt AIi Mohamed Shein wakifatilia ibada ya misa ya kumuaga Prof. Matthew Luhanga.
Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Ali Mohamed Shein, akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa Prof. Mathew Luhanga.
Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania ambaye pia alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Barnabas Samatta akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la Marehemu Profesa Matthew Luhanga.
JUMUIYA ya Chuo Kikuu Mzumbe watamuenzi Profesa Matthew Luhanga kama kiongozi wao na mwana mageuzi kwa kuwaweka kwenye projectory na kuwapa mbinu ya kuendelea kufanya mapinduzi makubwa na mageuzi katika Chuo kikuu Mzumbe.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka ameyasema hayo leo Septemba 20, 2021 wakati wa kutoa salamu za pole wakati wa ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Matthew Luhanga alifarikia dunia Septemba 16,2021 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokiwa akipatiwa matibabu.
Prof. Kusiluka amesema kuwa kuna andiko lake lililenga katika mapinduzi ya nne ya viwanda, ili chuo iwezekane kishiriki kikamilifu katika mapinduzi ya nne ya viwanda kwa kutumia fursa zilizopo katika uchumi wa kidijitali, wanataaluma na wanazuoni watahitajika kufanya tafiti ili kutoa majibu yatakayo itayarisha nchi kuweza kufaidi mapinduzi ya nne ya viwanda.
Ameongeza kuwa, Marehemu Prof. Luhanga aliendelea na mageuzi kwa miaka mitano katika chuo kikuu Mzumbe, katika miaka hiyo Mitano kulikuwa na mageuzi ya Miundombinu ya elimu, mageuzi katika mifumo ya utawala na mageuzi makubwa yanayoendelezwa na jumuiya ya chuo hicho.
“Tutaendelea kufanya yote aliyotuasa kuyafanya ili chuo chetu ambacho ni chuo cha umma cha watanzania pamoja na wenzetu tunaoshirikiana nao ili tuweze kusonga mbele na tukisonga mbele chuo kimoja, vyuo vyote na watanzania wanapata faida kubwa." Amesema Prof. Kusiluka
Hata hivyo Prof. Kusiluka amesema kuwa Marehemu kuna kitu ambacho amewaachia wakifanye na wasipokitekeleza watamnyima usingizi huko alipo na wakikifanya kwa ukamilifu anadhani kuwa roho yake italala kwa amani.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, CPA. Pius Maneno amesema kuwa Prof. Luhanga atakumbukwa na wadau wote wa elimu katika mchango wake katika tasnia ya elimu kwai alikuwa Mwadilifu, mcheshi mtu mwenye msimamo wa kipekee katika yale aliyokuwa akiamini na kuyafanya.
“Ni Msimamizi mkubwa wa ubora na mwenye kujituma sana katika kazi yake alikuwa kiongozi mwenye maono makubwa katika kipindi kifupi alichofanya kazi na chuo kikuu Mzumbe, amechangia katika mabadiliko makubwa ya kitaasisi katika chuo chetu kwa kushirikiana na wajumbe wenzake wa baraza.Alisisitiza CPA. Maneno
Ameongeza kuwa moja ya ajenda zake zitakazokumbukwa ni msisitizo wake katika kujiandaa kushiriki katika mapinduzi ya nne ya viwanda. Ametuachia hazina kubwa ya mawazo na maono ambapo chuo kikuu Mzumbe kitayaenzi katika uongozi wake na kuyafanikisha.
Marehemu Prof. Luhanga aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa
Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe Agosti 2016 kwa kipindi cha kwanza cha miaka minne
alichokimaliza Agosti, 2020 na Septemba 2020 kaliteuliwa tena kuendelea wadhifa
huo kwa awamu ya pili, anatafajia kuzikwa Septemba 21, 2021 katika makaburi ya
Kondo, Kunduchi Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment