HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 04, 2021

Kamishna Mstaafu Boaz alishauri Jeshi la Polisi kuwekeza kwenye teknolojia kukabiliana na uhalifu

 


 Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi aliyekuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Robert Boaz amelishauri jeshi hilo kuwekeza katika teknolojia ili kukabiliana na mabadilko ya matukio ya uhalifu nchini.

Ushauri huo ameutoa jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika Hafla ya kumuaga iliyofanyika Katika Chuo cha Polisi kilichopo Kurasini jijini humo.

Amesema kuwa jeshi hilo lintakiwa kutumia mbinu mpya za kupambana na uhalifu kwa kutumia mifumo ya teknolojia kwani matukio ya uhalifu yanabadilika kutokana maendeleo teknolojia yanayoenendelea kutokea duniani.

" Jeshi la Polisi liwekeze katika teknolojia maana uhalifu unabadilika likifanya hivyo itakuwa rahisi kupambana na wahalifu wanaotumia mbinu mpya zinazoendana na teknolojia, " amesema Kamishna Mstaafu Boaz.

Amewaisitiza askari ambao bado wanalitumikia jeshi hilo kuendelea kuwahudumia wanachi kwa upendo na kufanya kazi yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu, weledi pamoja na maadili.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi hilo Tanzania IGP Simon Sirro amesema licha ya matukio ya hivi karibuni nchi bado iko katika hali ya amani na usalama hivyo wananchi waendelee kufanya shughuli zao bila wasiwasi.

IGP Sirro amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikano kwa jeshi hilo kwa kutoa taarifa pale wanapohisi  matukio ya uhalifu kwani watalisaidia kukabiliana na matukio hayo.

Inspekta Jenerali huyo amewaomba wazazi na walezi kuwapa watoto malezi malezi bora yatakayosaidia kujenga taifa lenye watu wenye maadili hali itakayochangia kupunguza vitendo vya uhalifu.

No comments:

Post a Comment

Pages