Na John Dande, Dar es Salaam
KATIKA kuelekea kwenye Tamasha la Kumshukuru Mungu litakalofanyika Oktoba 31 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, waimbaji watakaoshiriki katika tamasha hilo tayari wameingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya tamasha hilo.
Waimbaji waliotambulishwa leo ni Boniface Mwaitege na Christopher Mwahangila. Wengine waliothibitisha kushiriki ni pamoja na Upendo Nkone, Jessica Honore, Messi Chengula na Enock Jonas.
Mkurugezi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama, ambao ndio waratibu wa tamasha hilo, amesema mpaka sasa maandalizi yanakwenda vizuri katika kuelekea kwenye tamasha la kumshukuru mungu.
"Nataka niwaeleze kwamba mambo yamezidi kupamba moto, yamezidi kuwa mazuri kuelekea Oktoba 31, waimbaji wengi wameendelea kuthibitisha kushiriki kwenye tamasha hili kubwa la kihistoria."
Tamasha hili linakuja baada ya miaka sita ya kutokuwepo kwa matasha yanayoratibiwa na Msama Promotion hivyo katika kuhakikisha wapenzi wa nyimbo za injili wanapata burudani safi, waimbaji watakaoshiriki ni wale wenye uwezo wa kutumia vyombo jukwaani 'Live' na sio CD.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 5 wakati akiwatambulisha waimbaji wa nyimbo za injili watakaopanda jukwaani katika Tamasha la Kumshukuru Mungu litakalofanyika Oktoba 31, 2021. Kushoto ni Mratibu wa Tamasha hilo, Emmanuel Mabisa na kulia ni mwimbaji wa nyimbo za injili, Mess Chengula. (Picha na John Dande).
No comments:
Post a Comment