September 30, 2021

MBIO ZA MWENGE WA UHURU KUKIMBIZWA KILOMETA 61 WILAYANI KYEWA MIRADI 10 KUZINDULIWA


Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu akizungumzia ujio wa mwenge wa uhuru.

 

Na Lydia Lugakila, Kyerwa

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera Rashid Mwaimu katika kikao maalum cha baraza la madiwani kilichofayika katika  ukumbi wa Rweru Plaza.

Mwaimu amesema kuwa  Mwenge wa uhuru utapokelewa oktoba 4, 2021 katika kata ya Itera kijiji cha Chanya mpakani mwa wilaya ya Karagwe na Kyerwa ambapo jumla ya miradi 10 itazinduliwa ikiwa ni pamoja na uwekaji mawe ya msingi katika baadhi ya miradi hiyo.

 Amesema kuwa mwenge huo utakimbizwa kwa takribani kilometa 61 katika wilaya hiyo na kuitaja miradi itakayozinduliwa kuwa ni pamoja na Ofisi ya taasisi ya kifedha CRDB Nkwenda yenye thamani ya shilingi bilioni 5, uzinduzi wa mradi wa maji wenye thamani ya sh milioni 246 pamoja na kutembelea mradi wa wajasiliamali wenye thamani ya sh milioni 5, uzinduzi wa jengo la mama na mtoto wenye thamani ya sh milioni 249 pamoja na miradi mingineyo.

Aidha mkuu huyo wa wilaya aimeitaja miradi itakayowekewa jiwe la msingi ni pamoja na barabara ya KIDO, Shule ya sekondari Isingiro yenye mradi wa vyumba 2 vya  madarasa vyenye thamani ya sh milioni 40.

Hata hivyo amewaomba wananchi wilayani humo kujitokeza kwa wingi kuupokea mwenge huo kwa shangwe kubwa.

No comments:

Post a Comment

Pages