September 29, 2021

NMB wazindua Akaunti ya Wekeza kuimarisha uwekaji akiba

 

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Wekeza Akaunti uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa, Janet Rwegasila na Mkuu wa Idara ya Bidhaa Benki ya NMB, Aloyse Maro. (Na Mpiga Picha Wetu).


Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya WEKEZA Akaunti uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa, Janet Rwegasila, Mkuu wa Idara ya Bidhaa Benki ya NMB, Aloyse Maro na kulia ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa, Beatice Mwambije.


Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kulia), akizindua huduma mpya ya Wekeza Akaunti uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa NMB, Janet Rwegasila, Mkuu wa Idara ya Bidhaa Benki ya NMB, Aloyse Maro na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalumu, Getrude Mallya. 


Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa tatu kulia), akizindua huduma mpya ya WEKEZA Akaunti uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Meneja Mauzo NMB, Darius Elius,  Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa NMB, Janet Rwegasila, Mkuu wa Idara ya Bidhaa Benki ya NMB, Aloyse Maro, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalumu, Getrude Mallya na kulia ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa, Beatice Mwambije.

 

 Na Mwandishi Wetu

 

BENKI ya NMB kwa mara nyingine imedhihirisha ubunifu wake kwa kuzindua akaunti ya dhamana ya muda mrefu inayoambatana na bima ya maisha bure.

 

Akaunti hiyo iliyopewa jina la ‘Wekeza’ ni ya kwanza ya aina yake katika soko nchini ambayo inatoa riba shindani na kuifanya NMB kuwa benki pekee yenye ubunifu huo katika huduma za kibenki yenye kutoa suluhu za kifedha kwa haraka.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 29, 2021, Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi Beki ya NMB, Filbert Mponzi alisema Akaunti ya Wekeza itavutia kwa maana ina kiwango cha riba hadi kufikia asilimia 12 kwa ambao watakuwa na uwekezaji wa muda mrefu. Ambapo alibainisha kiwango cha riba kitakwenda sambamba na idadi ya miaka ambayo mteja anataka kuwekeza.

 

“Tumeamua kuja na ubunifu huu kama ilivyo kawaida yetu lengo ni kuwafundisha Watanzania utamaduni wa kuweka akiba, ndiyo maana tumeruhusu kutoa fedha kwenye akaunti hiyo mara mbili kwa mwaka, Juni na Disemba kwa sababu tunafahamu huenda ikatokea dharura au kulipia ada za watoto,” alisema Mponzi.

 

Mponzia alisema: “Mtakumbuka hivi karibuni benki yetu ilipata tuzo sita zakimataifa mmojawapo kutoka jarida la ‘International Banker’ Benki ya NMB imekuwa benki bora kwa ubunifu wa bidhaa kwa wateja binafsi.

 

“Tunafurahia kumudu kuwapa wateja wetu njia nyingine salama na ya muda mrefu kuhifadhi fedha, ikumbukwe tunatoa huduma katika mazingira shindani zaidi, lakini kwa mara nyingine tunathibitisha kuwa tunaweza kuendelea kuleta bidhaa mpya zinazoongeza thamani kwa wateja.

 

“Tunajivunia zaidi huduma yetu ya Wekeza, tumejipanga kuhakikisha tunaongeza fursa kwa wateja wetu wakati tunaendelea kuwatia moyo kujizoesha utaratibu mzuri wa matumizi ya fedha.”  

 

Awali Mkuu wa Idara ya Bidhaa Benki ya NMB, Aloyce Maro alisema Akaunti ya Wekeza inatoa fursa kwa mteja kuanza kwa kuweka kiasi cha Shilingi 250,000 ambapo ataanza kwa kupata riba ya asilimia mbili kila baada ya miezi sita.

 

“Mteja atapata nafasi ya kuendelea kuweka akiba katika akaunti yake kadiri awezavyo, ambapo riba itaongezeka kulingana na kiasi alichonacho. Vilevile kutakuwa na huduma ya bima ya maisha bure itkayotolewa kulingana na kiasi cha akiba iliyopo hadi kufikia Shilingi Milioni 50, itawahusu wateja waliopata kilema cha maisha au kifo,” alisema Maro.

 

Aidha Maro aliongeza kuwa: “Tunataka wateja wetu waendelee kutuamini wakati tunasimamia amana zao, wakati huo huo tunawafundisha utamaduni wa kuhifadhi fedha kwa ustawi wa baadaye kifedha.”

 

Kiwango cha chini kuweka fedha kwenye akaunti ya Wekeza ni Shilingi 250,000 na umiliki wa amana unakuwa kati ya miaka sita hadi 20 (6-20), riba inayopatikana inalipwa mara mbili kwa mwaka, yaani mwezi Juni na Disemba. Vilevile akaunti inayo fursa ya kuongeza thamani ya uwekezaji kupitia njia mbalimbali ikiwemo matawi ya NMB, NMB Wakala na NMB Mkononi.

 

Akaunti ya Wekeza pia inatoa bima ya afya bure ikiwa mteja atafariki au kupata ulemavu wa kudumu, ambapo itakuwa ni mara mbili ya uwekezaji wake, kiwango cha chini ni Shilingi Milioni 2 hadi Shilingi Milioni 50.

No comments:

Post a Comment

Pages