September 18, 2021

Simba SC yaingia ubia wa kibiashara na ATCL




Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Klabu ya soka ya Simba SC na Shirika la Ndege Nchini (ATCL) wameingia mkataba wa ushirikiano wa kibiashara utakaowawezesha Simba SC kusafiri ndani na nje ya Tanzania kwa ndege za shirika hilo pekee.

Mbali na hilo mkataba huo wenye thmani ya Sh milioni 400 pia unatajwa kuwanufaisha mashabiki wa timu hiyo kwa kuwekea mfumo maalum wa kupata usafiri wa ndege kwa wepesi kwa ajili ya kwenda kuiunga mkono timu ya Simba SC inapocheza nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages