HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 10, 2021

KONGAMANO LA UTAFITI KUFANYIKA JIJINI DODOMA

Profesa Bernadeta Lillian.

 

 Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


KONGAMANO  la tatu la utafiti kwa maendeleo jumuishi litakalokusanya wadau mbalimbali wa Maendeleo watafiti na wanataaluma linatarajiwa kufanyika jijini Dodoma lengo  kuu la Kongamano hilo likiwa ni kujadili kwa pamoja jinsi ya kuboresha maisha ya watanzania na maendeleo ya nchi kwa ujumla.


Akizungumza leo jijini hapa Profesa Bernadeta Lillian amabaye ni Makamu Mkuu wa Chuo (Utafiti) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema Kongamano  hilo litaleta fursa ya kuwafahamisha wadau kuhusu matokeo ya utafiti katika miradi mabalimbali iliyofanywa na maprofesa wahadhiri na wanafaunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam. 



Aidha amesema katika Kongamano  hilo washiriki zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo wanadiplomasia, wabunge, watunga sera na wadau kutoka mashirika yasiokuwa yakiserikali.



Aidha alipoulizwa swali juu ya taarifa ya rushwa ya ngono katika chuo kikuu cha Dar es Salaam na tafiti zinasemaje juu ta tatizo hilo Profesa Bernadeta amesema nikweli tatizo hilo lipo chuoni hapo lakini wamekuwa wakikabiliana nalo kwa kujiwekea sheria mbalimbali za kinidhamu.



"Katika chuo chetu tataizo la rushwa ya ngono lipo lakini tumekuwa tukikabiliana nalo kwanza baisa chuo chetu kimekuwa kikiongozwa kwa sera mabalimbali ya masuala ya kijinsia na tumekuwa tukiwafatilia wanafunzi na waadhiri lengo likiwa ni kuhakikisha nidhamu inatawala chuoni hapa,"amesema 



Na kuongeza kusema kuwa"Wapo watumishi amabo tumeshawafukuza kazi kutokana na kubainika na vitendo hivyo kati chuo chetu cha Dar es Salaam pia tumekuwa tukiwapa elimu ya kijinsia wanafunzi wote wanaoingia mwaka wa kwanza chuoni ili waweze kujitambua  Profesa Bernadeta. 

No comments:

Post a Comment

Pages