January 26, 2022

BENKI YA CRDB YATEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akitangaza punguzo la riba katika mikopo kwa kundi la wakulima na wafanyakazi jijini Dar es Salaam.


Dar es Salaam, Tanzania

BENKI ya CRDB imetangaza punguzo la riba katika mikopo kwa kundi la wakulima pamoja na wafanyakazi.

 

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amesema kuwa punguzo hilo la riba limekuja kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kwa mabenki kuhusu kupunguza riba ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.

 

Nsekela amefafanua kuwa katika punguzo hilo riba ya mikopo ya kilimo imepungua hadi asilimia 9 kutoka asilimia 20 iliyokuwa hapo awali huku riba ya mikopo kwa wafanyakazi ikipungua kutoka asilimia 16 hadi 13, punguzo hilo la riba linatoa ahueni kwa wateja wa Benki ya CRDBkulipa mikopo yao kwa riba nafuu, viwango vya chini zaidi vya marejesho ya awali pamoja na kupata wigo mpana wa kukopo.

 

“Kwa ushirikiano mkubwa na Benki Kuu ya Tanzania ambae ndie msimamizi wa sekta ya benki nchini nchini, mwoshoni mwa mwaka jana tuliweza kukaa chini na kuanza utelelezaji wa mchakato wa kupitia upya riba za mikopo mbalimbali inayotolewa na benki uyetuna hivyo ninajivunia kuona leo hii tumekuja na suluhisho la kilio cha muda makiewahamasisha wateja na watanzania kuchangamkia fursa hiyo. 

 

Akiwa jijini Mwanza Juni 13, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alimuagiza Gavana wa Benki Kuu (BOT), Profesa Florens Luoga kukaa na Wizara ya Fedha na Mipango kujadiliana namna ya kupunguza kiwango cha riba katika mikopo inayotolewa benki mbalimbali nchini.

 

Rais Samia alisema riba kuwa juu ni  kikwazo kwa baadhi ya wawekezaji, wafanyabiashara na wananchi wa kipato cha chini kiasi cha kushindwa kukopa katika taasisi hizo za kifedha.

 

"Viwango vya riba vipo juu mno vishushwe angalau viwe kama asilimia 10 kushuka chini."

 

"Naagiza Benki Kuu kuanza kutengeneza mazingira ya kuhakikisha wanasimamia benki ndogo ili zitoe mkopo kwa vikundi na wananchi wenye kipato cha chini," alisema.

 

Pia, alizitaka benki hizo kuanza kutoa mkopo wa muda mrefu ili kuwawezesha wakopaji waanzishe miradi ikiwemo kufungua viwanda, mashamba ya kilimo.

No comments:

Post a Comment

Pages