HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

January 16, 2022

Binti wa miaka 18 auawa na mzazi mwenzie

 

 

Mama mzazi wa marehemu  Gaudensia Sinde (49),akiwa nyumabani kwake Kikuyu jijini Dodoma baada ya mazishi.

 

Betila Gasper enzi za uhai wake.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

CHRISTOPHER Kione anatuhumiwa kumuua mzazi mwenzie Betila Gasper(18), mkazi wa Kikuyu jijini Dodoma kwa kumpiga na kitu chenye ncha kali kichwani.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi  kwa masikitiko makubwa nyumbani kwake Kikuyu mama mzazi wa marehemu Gaudensia Sinde (49), amesema Januari 9, mwaka huu mtuhumiwa alikwenda nyumbani hapo kumchukua  Betila pamoja na mtoto wake kuelekea nyumbani kwake Mkonze.

Amesema mtuhumiwa alikuwa askari wa FFU  lakini alifukuzwa kazi alikuwa akiishi Mkonze na mdogo wake ,na walipofika huko nyumbani kwao alimtuma mdogo wake na  mtoto waende dukani.

Ameongeza kuwa kwamujibu wa mdogo wake baada ya kurudi hakumkuta kaka yake na mlango ulikuwa umefungua kwa nje  na piki piki (boda boda) haipo ndipo alipochungulia dirishani aliona mwili wa shemeji yake Betila  umelala kitandani.

Amesema baada ya kuona hivyo alienda kupanda pikipiki na kwenda  kutoa taarifa nyumbani kwa akina Betila na ndipo taarifa ikatolewa Polisi.

"Polisi walikuta mwili ulikuwa umelala kitandani una majeraha ya kupigwa na kitu chenye ncha kali,shingoni alikuwa ana majeraha kama alinyongwa na mikononi alikuwa amefungwa pingu," amesema mama mzazi wa marehemu kwa hudhuni.

Ameongeza kuwa Askari walipofika katika eneo la tukio wakajiuliza hizo pingu zimetoka wapi? na kwamba mwili ulichukukuliwa na kupelekwa chumba cha maiti tayari kwa taratibu za mazishi.

" Moyo wangu umeumia Sana  mwanangu amekufa kifo cha kikatili sana, ameshonwa majeraha kabla ya kuzikwa," ameeleza.

Amesema Betila alikuwa mtoto wake wa tatu na bàdo wanafuatilia Polisi lakini mpaka sasa mtuhumiwa bado hajakamatwa.

Kwa upande wake mdogo wa mtuhumiwa George Charles amesema siku ya tukio akiwa nyumbani alikuja mtuhumiwa wakiwa wameongozana na Betila (marehemu) na mtoto wao.

"Yule ni shemeji yangu, lakini  tangu krismasi nilikuwa sijamuona kuja pale nyumbani ila siku hiyo alikuja akiwa ameongozana  na kaka (mtuhumiwa) na mtoto wao," amesema

Ameongeza kuwa ndipo kaka yake  akamwambia  aende dukani akamnunulie mtoto juisi  na kudai kwamva  alikuwa na mazungumzo na shemeji  yake.

"Nikamchukua mtoto, nikaenda dukani  nikanunua juisi nikawa nacheza cheza na mtoto ili kupoteza muda, baada ya dakika 10 mtoto akaanza kulia anamtaka mama yake, nikaamua kuondoka pale dukani kurudi nyumbani," amesema.

Charles ameeleza kuwa alipofika nyumbani hakuona pikipiki ambayo kabla ya kwenda dukani alikuwa ameipaki nje.

" Nikachungulia dirishani nikaona  shemeji  amelala kitandani, hapo inikahisi kitu sio cha kawaida, wakati huo mtoto alikuwa akilia sana , nikaamua kumpeleka mtoto kwa babu yake Kikuyu na kuwaeleza juu ya sintofahamu niliyoikuta wakasema tupite Polisi tukatoe taarifa kabla ya kurudi tena huko," amesema.

Amefafanua kuwa walikwenda kutoa taarifa Polisi na wakaondoka na gari hadi nyumbani hapo na kufungua mlango, kuingia ndani na kukuta marehemu akiwa amelala kitandani akiwa na jeraha kubwa kichwani na baadae hatua za kipolisi zilifuata ikiwa ni pamija na  kuchukua mwili wa marehemu.

Mmoja wa marafiki wa marehemu Bahati Msanjila amesema alimfahamu marehemu muda mrefu.

"Alikuwa ni jirani yetu hapa nyumbani na nilikuwa namchukulia kama mdogo wangu kwa kuwa tumeishi kwa ukaribu tukishirikiana kwa mambo mengi  hata kwenye send off yangu alikua ni moja kati ya maids wangu" amesema.

"Alikua mpole, mkarimu hajui kukasirika yaani hata huyo mwenzie kama walipishana kauli akafanya kumdhuru kamkosea binti wa watu. Nimeumia sana marehemu kaacha mtoto mdogo wa miaka mitatu au minne ambaye bàdo alikuwa anahitaji malezi ya mama yake," amesema.

No comments:

Post a Comment

Pages