HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 27, 2022

Jeshi la Polisi nchini lapewa siku saba kuwakamata waliofanya mauaji ya familia moja ya watu watano


Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango akizungumza katika kaya iliyopoteza watu watano wa familia moja kwa mauaji ya kikatili alipoenda kutoa pole kwa niaba ya Rais Samia.

 

NaAsha Mwakyonde, Dodoma

MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango ametoa siku saba (7),kwa Jeshi la polisi nchini na Idara  zake kukatwa kwa waliofanya mauaji  ya watu watano  wa familia moja yaliyofanyika katika Kata ya Zanka Wilayani Bahi jijini Dodoma kuanzia leo na ifike mezani kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan kuanzia leo.

Pia Dk.Mpango amewataka viongozi wa dini kuisaidia serikali kuwakumbusha waumini wao kuwa hakuna mwanadamu wa kutoa uhai wa mtu mwingine na kwamba kama kunatatizo wazee wanaweza kusuluhisha.

Mauaji hayo yaliyofanywa na watu wasiojulikana  yametokea mwishoni mwa wiki iloyopita  ambapo maziko yamefanyika siku ya Jumapili.

Dk.Mpango ameyasema hayo leo Januari 26,2022 alipoenda kutoa pole kwa familia hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesem Rais amesononeshwa  na mauaji hayo.

Amesema kiongozi na Amiri Jeshi Mkuu Samia amechoka kuongoza nchi yenye mauati ya kutisha ambayo yanatia doa taswira ya nchi na kwamba serikali imetoa maelekezo hayo  yafanyike mara moja.

" Tukio hili linasikitisha, linaumiza sana. Nimefika hapa kwa niaba ya Rais Samia kuwapa pole ambao mmepoteza watoto wenu kikatili, Mwenyezi Mungu awatie nguvu," amesema Makamu wa Rais Dk. Mpango.

Dk. Mpango amesema tukio hilo halikubaliki hapa nchini inawwzekanaje hata majirani kujua na kwamba Jeshi hilo lifanye kazi mara moja na pia Idara ya upelelezi ifanya kazi saa 24 hadi wahalifu wa mauaji hayo wapatikane.

" Kamanda wa Polisi wa Dodoma nifikishie salamau kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini  (IGP),Simon Siro  haya mauaji nchi nzima yakafanyiwe kazi sawa sawa, nimesikia leo baadhi ya watuhumiwa wa mauaji ya Mtwara ni polisi hatuwezi kwenda namna hii kama Polisi, kule Mbeya mwanajeshi kamuua baba yake na Arusha mtoto wa kike kamuua mama yake. Jeshi la Polisi lijisafishe linafanyakazi nzuri lakini wapo baadhi yao wanalichafua," amesema.

" Kama Jeshi la Polisi  hatuwezi kuongoza nchi mauaji kila mahali tumechoka, miili ilikaa siku tatu, watendaji, wenyeviti wa serikali ya mtaa, ndugu na majirani hawakujua,"amesema Dk. Mpango.

Amesema Jeshi la Polisi liwasake  mara moja waliofanya mauaji  ni unyama  wa hali ya juu nchi ya Tanzania ni ya amani inapotea hivi hivi haiwezekani.

Dk. Mpango ameeleza kuwa jeshi la Polisi na idara zake wafanye kazi usiku na mchana kuzuia mauaji yanayoenfelea nchini.

Makamu huyo wa Rais ameongeza kuwa wazee waliowapoteza familia yao itawachukua muda mrefu machozi yao kukauka.

Amesema kuna tatizo kubwa majirani hata kufika, viongozi wa mtaa , mjumbe wa nyumba kumi, wa Kijiji hadi miili inaharibika.

" Nawasihi mikoa yote hapa nchini  lazima tupendane penye tatizo tukae tupatane. Mkuu wa Wilaya atarudi kukaa kikao cha ulinzi na usalama ," amesema.

Aidha amewataka viongozi ngazi zote kuanzia chini kufanya mikutano ya mara kwa mara kwa lengo la kuwabaini wahalifu pindi wanapokuwa na viashiria vya uhalifu.

No comments:

Post a Comment

Pages