HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

January 13, 2022

Maige: Nachukua fomu ya kugombea Uspika kwa kuwa ni haki ya kikatiba


Aliyewahi kuwa Waziri wa maliasili na utalii na Mbunge wa Msalala Mkoani Shinyanga Ezekiel Maige, akizungumza na waandishi wa habari mara baada kukabidhiwa fomu ya kuwania nafasi ya Spika wa Bunge.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

ALIYEWAHI kuwa Waziri wa maliasili na utalii na Mbunge wa Msalala Mkoani Shinyanga Ezekiel Maige, amejitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kukiwakilisha Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamuhiri ya Muungano wa Tanzania.

Hatua ya kuchukua fomu inatokana na nafasi hiyo kuwa wazi baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge  hilo na Mbunge wa Kongwa Job Ndugai kujiuzulu.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo Maige amesema kuqa ana historia nzuri kwa  chama chake ambapo alijiunga akiwa na umri wa miaka 19 hivyo ana uwezo wa kukiwakilisha vema katika kuleta maendeleo ya nchi hasa katika kupambana na Umaskini, Ujinga na Maradhi.

Maige amesema ana uzoefu katika uongozi na Bunge hilo kwa kuwa alilitumikia kwa zaidi ya miaka 13 na kwamba anauzoefu mkubwa na wabunge kiutendaji.

Maige ameeleza kuwa lengo  kuwania nafasi hiyo ni kutekeleza haki ya kikatiba ya chama cha CCM ikiwemo za kuitumikia nchi na watu wake na kujitolea kwa nafasi kuondoa umaskini.

“Kama mwanachama nitatekeleza ahadi zote na endapo nitafanikiwa katika hili naahidi kutoa ushirikiano katika Bunge hususan kwenye mambo ya sheria," amesema Maige.

No comments:

Post a Comment

Pages