Mgombea nafasi ya spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Wilaya Bunda Mkoa wa Mara Emmanuel Mng'arwe ambaye pia ni Wakili Msomi wa Kujitegemea akizuzungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
MGOMBEA wa nafasi ya spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Wilaya Bunda Mkoa wa Mara Emmanuel Mng'arwe ambaye pia ni Wakili Msomi wa Kujitegemea amesema amejitasimini na kuona kuwa anafaa kugombea nafasi hiyo.
Chama hicho kilifungua pazia la kupokea maombi ya kugombea nafasi hiyo Januari 10 hadi 15 ambayo iliachwa wazi na aliyekuwa spika wa Bunge hilo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kongwa Job Ndugai aliyejiuzulu hivi karibuni.
Akizungumza leo Januari 13, 2022 mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo Mng'arwe amesema kuwa katiba inaruhusu mtu yoyote kugombea nafasi ya Spika kama ni mwanachama wa chama hiyo kwa mujibu wa katiba.
Wakili huyo msomi ameonngeza kuwa endapo atapata nafasi hiyo atahakikisha anatenda haki ili wananchi wapate maendeleo ya kiuchumi yanayotokana na kiongozi mwenye kiwango.
" Mimi ni mwanasheria kitaaluma na kwa kuwa Bunge ni chombo kinachotunga sheria nitakuwa mtu sahihi na natosha kuwa Spika wa Bunge kijana," amesema mgombea huyo.




No comments:
Post a Comment