HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

January 06, 2022

Washindi 100 wa NMB MastaBata wanyakua 10m/-


Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite, akizungumza na waandishi wa habari kabla ya droo ya kwanza ya Kampeni ya ‘NMB MastaBata Kivyako Vyako’ iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Kadi, Manfred Kayala, wa pili kushoto ni Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Joram Mtafya na kulia ni Afisa wa NMB Idara ya Kadi, Doreen Masonda. (Na Mpiga Picha Wetu).
 
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite, akibonyeza kitufe cha kompyuta kumtafuta mshindi wa droo ya NMB MastaBata Kivyako Vyako iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Kadi, Manfred Kayala na Katikati ni Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Jorama Mtafya.

Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite, akizungumza na mshindi wa droo ya ‘NMB MastaBata Kivyako Vyako’ iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Joram Mtafya na kulia ni Afisa wa NMB Idara ya Kadi, Doreen Masonda.
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Kadi wa Benki ya NMB, Manfred Kayala, akizungumza na mmoja wa wateja walioshinda katika droo ya kwanza ya Kampeni ya ‘NMB MastaBata Kivyako Vyako’ iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite na kushoto ni Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Joram Mtafya. 
 
 
Na Mwandishi Wetu

Wateja 100 wa kwanza wa kampeni ya NMB MastaBata-Kivyako Vyako walipatikana leo nakuzawadiwa pesa taslimu TZS 100,000 kila mmoja nataasisi hiyo kiongozi wa shughuli za kifedha nchini.

Washindi hao wamezawadiwa jumla ya TZS milioni 10.

Promosheni ya MastaBata-Kivyako Vyako ilizinduliwarasmi katikati ya mwezi Disemba mwaka jana kwa lengola kuchagiza matumizi ya kadi za malipo za Mastercardkama sehemu ya mchango wa NMB katika juhudi zataifa za kujenga uchumi usiotegemea sana fedhataslimu.

NMB pia inatumia kampeni hii ya kuendeleza uchumi wakidijitali kurudisha fadhila kwa wateja wake waaminifuambao wamekuwa ni muhili muhimu wa safari yake yamabadiliko ya kidijitali.

 Akizungumza wakati wa droo ya kuwapata washindi wakwanza wa MastaBata-Kivyako Vyako, MenejaMwandamizi wa Wateja Binafsi wa NMB, Bw. Ali Ngingite, alisema zaidi ya TZS milioni 200 zitanyakuliwakwenye kampeni hii ya miezi mitatu.

“Hili ni toleo la tatu la kampeni za MastaBata zilizoanzarasmi mwaka 2018 kuwahamasisha wateja na wasiowateja wa Benki ya NMB kutumia kadi za Mastercard wanapofanya malipo na miamala kupitia intaneti,” mtaalumu huyo wa mikopo binafsi alisema.

“Kama watangulizi wake, promosheni ya MastaBata-Kivyako Vyako pia ina lengo la kuwatambua nakuwazawadia wateja wetu waaminifu kwa kuendeleakutumia huduma zetu,” Bw Ngingite aliongeza nakutabainisha kuwa zitakuwepo pia droo za kila mwezi naile kubwa ya mwisho.

Wakati washindi 100 wa kila wiki watashinda TZS 100,000 kila mmoja, 25 watanyakua TZS 1,000,000 kila mwezi na 30 wa mwisho watashinda jumla ya TZS milioni 90.

No comments:

Post a Comment

Pages