HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 13, 2022

Mkataba wa Kimataifa wa Plastiki ni hatua ya kihistoria katika kupambana na uchafuzi wa plastiki


KATIKA  kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na taka za  plastiki, Mtandao wa Mkataba wa Kimataifa wa Plastiki umetoa wito kwa nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania, kutambua thamani ya sekta isiyo rasmi, hasa vyama vya ushirika vya waokota taka kama sekta muhimu katika kuondokana na janga hilo.

Hii ni mara ya kwanza ambapo jukumu la waokota taka kukubaliwa katika azimio la mazingira kama moja ya hatua za  maendeleo ya msingi katika kukabiliana na mabadiliko  ya tabia nchi yanayosababishwa na taka zitokanazo na bidhaa za plastiki.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotplewa jana katika vyombo vya habari mtandao huo wa mkataba wa kimataifa unawatambua waokota taka hao sio tu kama washikadau,  lakini kama vyanzo muhimu vya maarifa na utaalamu ambao ushiriki wao utakuwa muhimu katika kutatua mgogoro huo wa plastiki.

"Mapema mwezi huu, katika Bunge la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEA), pande zote zilikubaliana juu ya mamlaka ya kujadili mkataba unaofunga kisheria kushughulikia mzunguko kamili wa maisha ya plastiki kutoka kwa uzalishaji hadi utupaji," alieleza Mkurugenzi Mkuu  Mtendaji wa Taasisi ya Nipe Fagio, Bi Ana Le Rocha katika taarifa yake hiyo.

"Itaathiri mustakabali wa mamilioni ya watu,” aaliongeza Bi Rocha.

Alisema kwamba Mkataba huo unaonyesha jinsi mzozo wa plastiki unavyoongezeka haraka na jinsi harakati zinazoendeshwa na raia kukabiliana nazo zimekuwa na nguvu.

"Sasa tuna dhamira ya kimataifa kukomesha uchafuzi wa plastiki," alibainisha Bi Rocha.

 Alifafanua kuwa wanachama katika Bunge la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEA) walikuwa wamekubali kufanyia kazi mpango huo ambao utatayarishwa na kuidhinishwa katika miaka miwili ijayo na Kamati ya Kimataifa ya Majadiliano (INC).

Alisema Mkataba wa Kimataifa wa Plastiki utajiunga na Itifaki ya Montreal na Mkataba wa Hali ya Hewa wa Paris kama mojawapo ya sheria muhimu za kimataifa za mazingira katika historia ya dunia.

Mkurugenzi Mkuu huyo Mtendaji anafafanua zaidi kwamba Muungano wa Kimataifa wa Njia Mbadala za Kuchoma moto (GAIA) na Vuguvugu la Kuachana na Plastiki zinasisitiza kwamba ushindi huu ni hitimisho la miaka mingi ya kupanga bila kuchoka kote ulimwenguni kufichua wigo kamili wa mgogoro wa uchafuzi wa plastiki, na hitaji la hatua ya haraka ya kimataifa.

Bi Roche anasema kuwa usaidizi wa mkataba wa kimataifa wa Plastiki ni mkubwa sana - zaidi ya vikundi 1,000 vya mashirika ya kiraia, wanasayansi 450, na zaidi ya watu milioni moja ulimwenguni wamejiunga na wito huo.
Amesema Makubaliano ya mwisho kwa kiasi kikubwa yanaonyesha vipaumbele vya mashirika ya kiraia kwa mkataba:

"Mkataba unapaswa kufunika uchafuzi wote wa plastiki, katika mazingira yoyote au mfumo wa ikolojia. Huu ni upanuzi muhimu wa mamlaka kutoka kwa dhana za awali za 

"plastiki za baharini" ambazo zingepunguza kwa kiasi kikubwa upeo na athari za mkataba,"alisema mkurugenzi mkuu huyo mtendaji.

Alisema kuwa mkataba huo utakuwa wa kisheria na kwamba vitendo vya hiari vinaweza kukamilisha vitendo vya lazima, lakini sio kuchukua nafasi yao.

Alisema kwamba mkataba huo utashughulikia mzunguko kamili wa maisha ya plastiki kutoka kwenye kisima ambapo mafuta na gesi hutolewa, kupitia uzalishaji na matumizi yake, hadi taka za baada ya mtumiaji.

Alisema mkataba huo utaambatana na usaidizi wa kifedha na kiufundi, ikiwa ni pamoja na shirika la kisayansi la kuushauri, na uwezekano wa mfuko wa kimataifa wa kujitolea - maelezo yameachwa kwa mchakato wa mazungumzo ya mkataba.

"Labda kikubwa zaidi, mamlaka inapendekeza hatua za kukabiliana na uzalishaji wa plastiki, ambao hadi sasa unakadiriwa kuwa karibu mara nne ifikapo 2050, na kuchukua 10 -13% ya bajeti ya kimataifa ya kaboni, na kuhatarisha hali ya hewa yetu,"alisema mkurugenzi mkuu huyo mtendaji.

"Tunaahidi kwamba mamlaka itaangalia plastiki katika mzunguko wake wote wa maisha, na kutuondoa kutoka kwa afua zenye shida za mwisho kama uchomaji taka, na badala yake kushughulikia suala hilo juu zaidi, katika awamu yake ya uzalishaji," kwa pande wake Mratibu wa GAIA  Afrika  Niven Reddy alisema.

"Hatua hii haingeweza kutokea bila vuguvugu la kimataifa kusukuma wafanya maamuzi kila hatua." aliongeza Niven.


No comments:

Post a Comment

Pages