Baadhi ya vitu walivyokabidhi wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa ajili ya kuwafariji watoto waliopo katika Mahabusu ya Upanga ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Mkuu wa Idara Masomo ya Utawala, Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Mary Rutenge, akimkabidhi Meneja wa Mahabusu ya Watoto - Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Darius Kalijongo baadhi yavitu vilivyotolewa na wanawake wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam. Kulia ni Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, Chuo
Kikuu Mzumbe, Prof. Honest Ngowi. (Na Mpigapicha Wetu).
Akizungumza
wakati walipotembelea kituo hicho, Mkuu wa Kitengo cha Masomo ya
Utawala, Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Mary Rutenge amesema
watoto waliopo katika Mahabusu ya Upanga wanatakiwa kupendwa na kujaliwa
kama watoto wengine.
Chuo Kikuu Mzumbe kuwasaidia watoto waliopo katika Mahabusu ya Watoto Upanga kutimiza ndoto na kutoa elimu ya biashara.
Akizungumza
wakati walipotembelea Mahabusu hiyo Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, Chuo
Kikuu Mzumbe, Prof. Honest Ngowi, amesema kuwa watoto wengi
wamesema malengo yao ni kuwa wafanyabiashara mbalimbali hivyo kama chuo
watapanga ratiba kwa ajili ya kuwapa elimu ya biashara watoto walio
katika mahabusu hiyo.
Kwa
upande wake Meneja wa Mahabusu ya Watoto - Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Darius Kalijongo amesema
kuwa watoto waliopo katika mahabusu hiyo wanaweza kila kitu
wanachofundishwa na walezi wao, hivyo wanabadilika kila siku kutokana na
ushauri wanaupata.
Amesema
watoto waliopo katika Mahabusu hiyo wanafundishwa mambo mbalimbali
ikiwemo msaada wa kisaikolojia pamoja na kupewa Upendo, Kutambuliwa,
kupewa usalama, Kukubalika, Kusifiwa pale wanapofanya vizuri,
Kuheshimiwa, Kushirikishwa, Kuaminiwa, Kulindwa na kupewa fursa ya
Kucheza.
No comments:
Post a Comment