Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi Ajira, Vijana na wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako amepiga marufuku kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini tabia ya kuwaweka ndani watumishi wa umma wenye makosa yasiyo ya jinai.
Prof. Ndalichako amepiga marufuku hiyo leo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa baraza kuu la shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ambapo amesema haipaswi kuwekwa ndani watumishi wa umma kwa makossa yasiyo ya jinai kwani pamekuwa na tabia ya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kuwaweka ndani watumishi wa umma kwa makossa yasiyo ya jinai.
Hivyo,amesema makossa ya kiutendaji kwa watumishi yachukuliwe hatua sehemu za kazi.
Kuhusu suala la Kuweka wafanyakazi ndani kwa makosa yasiyokuwa ya kijinai amesema serikali imeshatoa miongozo kwa wakuu wa mikoa na wilaya wasiweke watumishi ndani kwa makosa ambayo siyo ya jinai.
Aidha Prof. Ndalichako amewaagiza waajiri wote nchini kuhakikisha vikao vya mabaraza ya wafanyakazi vifanyike kwa mujibu wa matakwa ya kisheria ikiwemo kulipa posho stahiki kwa wafanyakazi.
Rais wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya amesema kuna haja kwa serikali kutekeleza ipasavyo kuwarejesha kazini watumishi wa darasa la saba kwani kuna baadhi ya taasisi zimekuwa zikiwakataa na kuwanyima stahiki.
Nyamhokya amesema TUCTA inaahidi kuendeleza kumpa ushirikiano Rais Samia na wanaamini katika sherehe za mei MOSI za mwaka huu atafanya kitu kwa wafanyakazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya wanawake wa shirikisho hilo Rehema Ludanga akibainisha kuwa bado kuna changamoto ya utekelezaji wa sheria ya mkataba wa kazi.
Ludanga amewaasa wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii ili iwe rahisi kwa serikali kungalia namna bora ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi.
No comments:
Post a Comment