Mchezaji Joseph Mwambipile wa timu ya Uchukuzi SC akirusha tufe katika mashindano ya kombe la Mei Mosi Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma na kuibuka mshindi wa pili kwa kurusha umbali wa mita 10:70; mshindi wa kwanza na Francis Tabu wa Wizara ya Mambo ya Ndani (11:00) na watatu ni Lioitiko Mwasere wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mita 10:30.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU za Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Mambo ya Ndani zimeng’ara katika michezo wa riadha kwa kuibuka washindi wa kwanza na pili, michezo iliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini hapa.
TAMISEMI imeshiriki mbio mita 100, 200, 400, 800, 1,500, 3,000, kupokezana vijiti za mita 100x4; na kurusha tufe kwa wanawake na wanaume wamejikusanyia alama 50 baada ya kupata medali za dhahabu, fedha na shaba..
Wachezaji Nuru Mkomsoh amekuwa wa pili kwa wanawake na kutwaa medali ya fedha katika mbio za mita 3,000; wakati Salome Ruvanda naye katwaa fedha katika mita 100; Atson Mbugi na Nuru Mhomsoh wametaa medali za fedha katika mbio za mita 1,500; huku Tegemea Mbogela katwaa medali ya dhahabu kwa wanawake katika mita 400; na Akson na Nuru tena wametwaa medali ya fedha katika mbio za mita 800.
Pia Atson aliyekuwa akiongoza ametwaa medali ya dhahabu katika mbio za mita 200, na Salome tena akitwaa medali ya fedha katika mita 200 kwa upande wa wanawake; naye Neema Chongoro katwaa medali ya dhahabu katika mchezo wa kurusha tufe huku kaka yake Liuitiko Mwasere ametwaa medali ya shaba katika mchezo huo.
Timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani iliyoongozwa na wanariadha wake wa kimataifa walishika nafasi ya pili kwa kujikusanyia alama 35, ambao ni Mariam Salum na Basil John wametwaa medali za dhahabu katika mita 3,000; 1,500 na 800; pia Mariam tena ametwaa medali ya dhahabu katika mita 100 na 200; na Basil katwaa tena medalI ya dhahabu katika mita 400.
Timu ya Uchukuzi SC wameshika nafasi ya tatu kwa kupata alama 29, ambapo wanariadha wake Shagi Luguwa kutwaa medali ya dhahabu katika mbio za mita 100 wanaume; huku Gift Kisaka akitwaa medali ya shaba katika mbio za mita 1,500; naye Aidan Adrian katwaa medali ya fedha katika mbio za mita 400; na Anna Charles katwaa medali ya shaba katika mbio za mita 400.
Katika mbio za mita 200 Baraka Kinguru katwaa medali ya shaba; huku mchezo wa kupokezana vijiti kwa mita 100x4 timu ya Uchukuzi wametwaa medali ya fedha kwa wanawake na wanaume; wakati katika mchezo wa kurusha tufe Joseph Mwambipile ametwaa medali ya fedha na Daktari Hawa Senkoro ametwaa medali ya dhahabu kwa kuibuka wa kwanza katika mbio mita 100 kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 50. Dkt anamiaka 58.
Nayo timu ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) imeshika nafasi ya nne kwa kujikusanyia alama tano baada ya wachezaji wake Grace Mushi kutwaa medali ya shaba katika mbio za mita 3000, huku Grace tena akitwaa medali kama hiyo katika mita 800 na 1,500; wakati kwa upande wa wanaume Polycarp John katwaa medali ya fedha kwenye mbio za mita 100.
Halikadhalika timu za Wizara ya Maji na Wizara ya Kilimo zote zimefungana pointi nne kila mmoja; huku Wizara ya Maliasili na Utalii; Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC); Mzinga; Wakala wa Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) zote zina alama tatu kila mmoja.
Nayo Wizara ya Fedha na Mipango inaalama mbili baada ya wachezaji wake wenye umri mkubwa wa kuanzia miaka 50, Wazael Kallage na Suleiman Mohamed; wakipata medali za fedha na shaba; huku Msajili wa Hazina mwenye medali ya fedha iliyotwaliwa na Evelina Kwilemelu; nao Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Wizara ya Madini na Wizara ya Afya kila mmoja inaalama moja.
Michuano hiyo inaendelea leo kwa michezo ya jadi ya bao, karat ana draft itakayofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini hapa.
No comments:
Post a Comment