Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (kushoto) akianzisha harambee kusaidia watoto wanaosoma kwenye kitengo cha elimu maalum shuleni Shule ya Msingi Igunga. |
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (kulia) akizungumza kwenye maonesho hayo. |
Wanafunzi nao hawakubaki nyumba bali wajijitokeza kuchangia chochote kumuunga mkono Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga. |
Baadhi ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) pamoja na wadau wa elimu wakichangia chochote kusaidia wanafunzi wa Elimu Maalum katika Shule ya Msingi Igunga walipotembelea shule hiyo. |
Baadhi ya wanafunzi wa Elimu Maalum katika Shule ya Msingi Igunga wakiendelea na maonesho kwa wadau wa elimu, kuonesha uwezo wao katika ujifunzaji. |
WANACHAMA wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wanaoshiriki katika Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, wameguswa na maonesho ya watoto wenye mahitaji maalum waliyoyafanya mbele yao na kulazimika kuwachangia fedha zaidi ya shilingi laki sita ili iwasaidie katika ujifunzaji wao.
Wanafunzi hao wenye mahitaji maalum kutoka katika Shule ya Msingi Igunga pamoja na walimu wao walifanya maonesho kwa wanachama wa TENMET namna wanavyojifunza na matumizi ya vifaa vinavyowasaidia katika ujifunzaji wao, jambo ambalo liliwagusa wadau hao wa elimu walipoitembelea shule hiyo ikiwa ni mwendelezo wa Maadhimisho ya Juma la Elimu.
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga ndiye alieanza kuguswa na wanafunzi hao pamoja na walimu wao baada ya kuainisha changamoto zao, jambo ambalo lilimlazimu kuendesha harambee ya ghafla iliyoungwa mkono na wadau wote wa elimu waliokuwa katika ziara hiyo kabla ya kuanza kujitolea chochote kwa kila mmoja.
"Binafsi nimeguswa na changamoto walizozitoa walimu wa kitengo hiki hasa upungufu wa vifaa vya kufundishia na nimevutiwa pia na juhudi wanazozionesha walimu na wanafunzi huku wakiendelea kufanya vizuri licha ya changamoto zao," alisema Bw. Wayoga akihamasisha kila mmoja kujitolea.
Wadau hao wa elimu walipata fursa ya kutembelea ujenzi ya bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum linalojengwa katika Shule ya Msingi Igunga na kuahidi kuwa watasaidia kiasi kidogo ili kuunga mkono juhudi hizo za Serikali kabla ya kuhitimisha shughuli za Maadhimisho ya Juma la Elimu za mwaka huu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Msingi Igunga, Bw. Issa Maulid akipokea fedha zilizochangishwa katika harambee hiyo, aliwashukuru wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania kwa moyo wao wa kuguswa na kujitolea kwao na kuahidi watahakikisha kiasi hicho cha fedha kinaelekezwa kutatua changamoto za watoto hao katika ujifunzaji.
Mashirika wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania waliotembelea shule hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya juma la elimu ni pamoja na Uwezo Tanzania, HakiElimu, Brac Maendeleo, REPSI, ADD International, ShuleDirect, Sense International, Malala Fund, WOWAP, Right to Play, CAMFED, WeWorld, Shule Bora, CASEE, AMUCTA, Pestalozzi Children’s Foundation, SAWO, CDO, Education Opportunity, Room to Read, Plan International, Lyra in Africa na Feed the children.
Mashirika mengine ni; KCBRP, CBIDO, KESUDE, KARUDECA, DRS, Beyond Giving, Mama Kevina Hope Children Centre, SALVE Regina, SMD, AWPD, Caritus Rulenge, Brothers of Charity, EOTAS, NELICO, MDREO, Sengerema CDH, Lake Victoria Disability Centre, St. Justin Center for Child with Disabilities, Children in Crossfire, Room to Read, AFRIWAG naTEN/MET Secretariat.
No comments:
Post a Comment