HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 09, 2022

KISENA WA UDART AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UTAKATISHAJI FEDHA


Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART), Robert Kisena (kulia) akiwa na washtakiwa wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha. (Na Mpiga Picha Wetu).

 

Na Mwandishi Wetu, Kisutu

 

MKURUGENZI wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam(UDART), Robert Kisena na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakikabiliwa kesi mbili tofauti  ikiwamo mashtaka  jumla 33 kati yake ya kutakatisha fedha zaidi ya Sh.Bilioni tano.

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Mahakimu  wawili   akiwamo, Hakimu Mkazi Mkuu Pamela Mazengo na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi, Godfrey Isaya.

Upande wa Jamhuri iliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Pius Hilla na Jackline Jantori waliwasomea mashtaka ambayo hawakutakiwa kujibu.


Katika kesi ya kwanza mbele ya Hakimu Isaya, Wakili Nyantori aliwataja washtakiwa kuwa ni Kisena, Mkurugenzi UDA na  UDART, Charles Selemani na Mtunza Fedha wa UDART, Tumaini Kulwa.


Katika kesi hiyo washtakiwa wanakabiliwa na jumla ya mashitaka 18 yakiwemi nane ya kutakatisha fedha jumla ya Shilingi 4,505,125,000, kusababisha hasara ya kiasi hicho na mashitaka mengine ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo.


Inadaiwa makosa hayo kati ya Agosti mosi 2015 na Desemba 2015 mahali tofauti Dar es Salaam.


Inadaiwa kuwa washtakiwa waliongoza genge la uhalifu na  kujipatia zaidi ya Sh. bilioni nne kutoka UDART.


Kati ya Juni 2015 na Aprili 30, 2016 walighushi nyaraka wakionesha UDART imeingia mkataba na Kampuni ya Maxcom Afrika Limited wa kusambaza kadi zenye thamani ya Sh bilioni 2.2 wakati si kweli.


Nyantori alidai katika shtaka lingine, Selemani anadaiwa kuwasilisha nyaraka hiyo huku akijua anadanganya, shtaka lingine Selemani anadaiwa kughushi nyaraka za kadi kuonyesha UDA imeingia mkataba na Maxcom na aliwasilisha barua hiyo NMB tawi la Benki House.


Shtaka la sita na saba Selemani,  anadaiwa kughushi barua nyingine kuonyesha waliingia mkataba UDA na Maxcom wa Sh 3,485,000,000 na kuwasilisha nyaraka hizo benki wakati si kweli.

Shtaka la nane Selemani kaghushi nyaraka kuonyesha UDART na Maxcom mkataba wameingia wa Sh milioni 425.

Inadaiwa shitaka la tisa aliwasilisha nyaraka za uongo, shitaka la kumi kusababisha hasara ya zaidi ya Sh bilioni 4 na mashitaka nane yaliyobakia wanadaiwa kutakatisha jumla ya Sh. 4,505,125,000.


Katika kesi ya pili mbele ya Hakimu Pamela inadaiwa Robert Kisena, Charles Selemani, John Mwala na Tumaini Kulwa, wanakabiliwa na mashtaka 15 yakiwemo tisa yakutakatisha fedha jumla ya Sh. milioni 750, kusababisha hasara ya kiasi hicho na makosa mengine ya kuhushi na kuwasilisha nyaka za uongo.


Katika shitaka la kwanza wanadaiwa kuratibu genge la uhalifu kati ya Mei 26 mwaka 2015 na Julai 10, 2016 Dar Salaam kwa makusudi waliratibu mpango wa kujipatia Sh milioni 750 kutoka UDART.


Mshtakiwa 1,2,4 wanadaiwa kughushi nyaraka ya kuhamisha fedha, wakionyesha UDART walihamisha Sh milioni 750 kwenda katika akaunti ya Kampuni ya Longway Engineering Limited.


Mshtakiwa wa nne anadaiwa kughushi hati ya kuhamisha fedha, Kisena anadaiwa kughushi miniti za Bodi ya Wakurugenzi iliwateua Kisena na Selemani kuwa watia saini wa katika akaunti ya UDART.

Kisena anadaiwa kuwasilisha nyaraka hiyi ya uongo NMB Tawi la Benki House na mashtaka tisa ya kutakatisha fedha jumla ya Sh milioni 750 ambazo walijihusisha na miamala hiyo ikiwemo kuhamisha fedha katika akaunti!za Kampuni ya Maxcom, Longway  na Kampuni ya Universal Cargo Trans shipment Holding Limited na fedha nyingine zilihamishiwa katika akaunti ya Kisena.

Pia wanadaiwa kuisababishia UDART hasara ya Sh milioni 750.
Upelelezi umekamilika, kesi zitatajwa Mei 23 mwaka huu, washtakiwa wote wamekwenda gereza la Segerea.
Kisena kwa mara ya pili anarudi gerezani kwa makosa ya utakatishaji, ambapo awali aliondolewa mashtaka hayo katika kesi nyingine akawa nje kwa dhamana.
Mwisho .

No comments:

Post a Comment

Pages