May 22, 2022

NIMR yazindua Maabara ya Utafiti Vinasaba vya Ugonjwa wa Malaria

Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifelo Sichalwe akizungumza katika Hafla ya Uzinduzi wa Maabara ya Utafiti wa Vinasaba vya Ugonjwa iliyofanyika katika Ofisi za NIMR, jijini Dar es Salaam.

 

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Serikali kupitia Taasisi yake ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)imesema itahakikisha inaongeza jitihada za kutokomeza Ugonjwa hatari wa Malaria ambao umendelea kuwa tishio na kusababisha vifo vingi.

Hayo yamesemwa Jijini humo wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Maabara ya Kufuatilia Vinasaba vya Ugonjwa wa Malaria na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt.Aifello Sichalwe amesema kwamba Maabara hiyo ni moja ya mkakati wa Wizara ya Afya kupitia Mpango wa kudhibiti Malaria Kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI).

Amebainisha kwamba Mradi huo wa Maabara ya Ufuatiliaji wa Vinasaba vya Malaria una lengo la kupata ushahidi wa kina juu ya chanzo kinachosababisha ugonjwa wa Malaria na kwamba utasaidia wataalamu wa masuala ya tafiti kupata suluhisho la Kukabiliana na ugonjwa wa Malaria.

"Utafiti huu wa Vinasaba vya Malaria niwa awamu ya kwanza kutekelezwa hapa Nchini ,na unafadhiliwa na wadau wetu wa maendeleo ikiwemo Umoja wa Ulaya(UN) na tunawaomba waendelee kufadhili ,pia tunaendelea kufanya mazungumzo na wadau wengine waweze kufadhili ile uwe endelevu nakufikia lengo tulilokusudia" amesema Dkt .Sichalwe.

 Dkt.Sichalwe amefafanua kuwa utafiti huo utasaidia kuwajengea uwezo NIMR Kwa kuzalisha takwimu za Vinasaba vya Malaria hapa nchini nakuzichakata Kisha wizara ya Afya itazitumia kufanya maamuzi ikiwemo kuandaa miongozo,kutunga sera  nakutekeleza mikakati mbalimbali ya kupambana na Malaria huku wakiwa na ushahidi wa kisayansi

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu( NIMR) Dkt.Khadij Malima amesema kwamba utafiti wa Vinasaba vya Ugonjwa wa Malaria umeanza tangu Mwezi Mei 2020 na utakamilika Mwezi Oktoba 2023 ambapo Kwa sasa umetekelezwa katika Mikoa kumi na tatu Nchini kote.

Ameitaja Mikoa hiyo kuwa ni Dar es salaam, Morogoro,Dodoma,Manyara,Pwani,Songwe,Ruvuma,Tabora,Tanga,Kagera,Mtwara,Kigoma,Mara.
nakusema kwamba wasimamizi Wakuu wa utafiti huo wa Vinasaba vya Malaria ni Waganga Wakuu wa Mikoa pamoja na Maafisa afya.

No comments:

Post a Comment

Pages