Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dk Venance Mwasse,akizungumza mara baada ya kusaini Mktaba mnono na Kampuni ya ABSA ya nchini Uswiss hafla iliyofanyika, jijini Dodoma.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
TANI 60,000 za Makaa ya Mawe huzalishwa kwa mwezi na kwa kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wake ambapo kiasi cha shilingi bilioni 250 zitazalishwa kama mapato katika Taifa kupitia mkataba wa mauziano wa tani hizo wa kampuni ya ABSA.
Haya yamesemwa leo Mei 10,2022 jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk.Venance Mwasse katika hafla ya utiaji saini mkataba wa Makaa ya Mawe ya Mkoa ya Songwe katika Mgodi wa Kabulo kupitia kampuni ya Kimataifa ya ABSA ambayo inajihusisha na Uchimbaji wa makaa ya Mawe nchini Uswiss, amesema mkataba wa mauziano utaongezeka zaidi mapato.
Dk. Mwasse ameeleza kuwa kusainiwa kwa mkataba huo ni matokeo ya mkakati wa kwanza wa uchimbaji wa Makaa ya Mawe ambapo tayari maandalizi yake yameshakamilika na mchakato kuanza hivyo mkataba huo ni mkubwa na ni wa kihistoria kwa nchi kwa kuwa utasaida kwenye masuala ya kiuchumi.
“Makaa hayo yatasafirishwa kutoka Kiwira hadi Bandari ya Mtwara na tayari magari 300 yatakayokiwa na madereva wawili kila moja yameandaliwa hivyo watakuwa 600 jumla, pia kutakuwa na nguvu kazi takribani watu 200,”.
‘Mkataba huu tutautekeleza kupitia vifungu tulivyokubaliana. Niwahakikishie ABSA kuwa mpo kwenye mikono salama na matokeo mazuri na huduma nzuri kwenu mtaziona,”amesema Dk.Mwasse.
Kwa upande wake Rais wa Kampuni ya ABSA, Bw.Gerges Schmickrath ameishukuru wizara kupitia STAMICO kwa kuaminiwa kuwekeza katika mradi wa makaa ya mawe. Amesema, mradi huo utakuwa na manufaa kwa watanzania kwa kuongeza pato la Taifa.
“Kupitia mkataba huu nawashukuru sana nchi ya Tanzania kwa kukubali maana hili suala tumelifanyia kazi miezi miwili hadi leo tumefikia kwenye uamuzi mzuri, tunaahidi tutafanya kazi nanyi maana yakiwepo mafanikio ni yetu sote so ya upande mmoja,”.
Naye Naibu Waziri wa Madini Dk.Steven Kiruswa amesema kuwa STAMICO itakusanya mapato wastani wa shilingi bilioni 4.16 kwa mwezi sawa na wastani wa shilingi bilioni 50 kwa mwaka.
"STAMICO itatoa ajira kwa vijana wa kitanzania zisizo za moja kwa moja 600 na fursa nyingine kupitia mradi huu. Nampongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dk. Mwasse na Menejimenti yake kwa kuwa wamekuwa wabunifu katika kutafuta masoko nje ya nchi," amesema.
Pia amesema kuwa ni matumaini yake makubaliano waliyokubaliana na kampuni ya ABSA yataleta tija katika nchi hizo na kuishukuru STAMICO kwa maamuzi ya kukubaliana kufanya biashara nchini ambapo itasaidia kuwapatia vijana ajira.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Drumlin Construction LTD ambaye ni msafirishaji wa makaa hayo nchini, Linus Seushy amesema kuwa wamejiandaa kuhakikisha kila kitu kinafanyika kama kilivyopangwa kwakuwa ni jambo la kihistoria kwa nchi.
No comments:
Post a Comment