HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 13, 2022

Wanawake wawa chachu ya uhifadhi wa misitu

 


Mtafiti Emmanuel Mtoto akielezea namna wanawake wanavyoshiriki katika usimamizi wa rasilimali misitu.


Afisa Kujengea Uwezo kutoka Katika Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania, Simon Lugazo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio ya tafiti.

 

Na Mwandishi Wetu, Morogoro


WANAWAKE wanaoishi katika jamii zenye uhifadhi simamizi shirikishi wa misitu wameonesha mabadiliko makubwa katika ushiriki, usimamizi na utumiaji wa rasilimali hizo.

Hayo yamesemwa na Ofisa Muhahamsishaji wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Saimon Lugazo wakati wa warsha iliyohusisha asasi mbalimba zinazojishughulisha na rasilimali misitu ambazo ni mwanachama wa Chama Cha Wafanyakazi za Misitu Tanzania (TFWG).

Lugazo alisema bado hakujakuwa na idadi ya sawa kati ya wanaume na wanawake, ila ni wazi kuwa wanawake wameamka hasa kwenye suala la umiliki wa ardhi, kufanya biashara za misitu na kushiriki katika vikundi vya hisa.
 
Kwa upande wake Dk.Mroto ambaye amehusika na utafiti alisema wapo wanawake ambao kwa sasa wameanza kujishughulisha na ukataji mkaa na kuwaweza kufungua miradi mbalimbali huku akishauri pia vijana nao wanahamasishwe vya kutosha kushiriki katika mradi.

Nao baadhi ya washiriki wa warsha hiyo akiwemo Marygoreth Lwekiza kutoka Shirika la Mpingo na Mandeleo (MCDI), Fadhila Kateta kutoka Jumuiko la Maliasili Tanzania na Isaya Sekibo kutoka Suredo wamesema kuwa miongoni mwa shughuli kubwa wanazozifanya ni kuhakikisha wanawake wanashirikishwa na wanashiriki vya kutoka katika shughuli za misitu.

Warsha hiyo ambayo imehusisha wanachama TFWG imewezeshwa na Mradi wa Kuhifadhi Misitu kupitia Biashara Endelevu ya Mazao ya Misitu (CoFoReST ) unaoendeshwa na TFCG wakishirikiana na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswizi (SDC).


No comments:

Post a Comment

Pages